Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Tuesday, October 23, 2012

MAJENGO YENYE KUMBUKUMBU IRINGA
PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE na MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI


MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI
 Mwana Kihesa huyu, alikuwa pilot wa ndege wa kwanza kutoka Kihesa, hii ilikuwa  mwanzoni mwa 1970. Mwamba alikuwa ni mtoto pekee wa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa Mzee Mnyamwani Kasongo. Mzee huyu mwenye asili ya ya mji wa  Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo alitinga Kihesa mwishon wa miaka ya 50.  Ukoo huu ilizimika duniani baada ya  Mwamba, Mama Mwamba, Mzee Mnyamwani, na mkee wake wa pili Binti Mussa wote kutangulia mbele ya haki. 

++++++++++++++++++++++++++++++++++
 PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE
 Mwana Kihesa huyu mtoto wa mama Se Uhagile ni msomi aliyebobea na ni muhadhiri pale chuo cha SAU ama kwa hakika kama si Profesor pekee toka Kihesa basi ni mmoja wa maprofesor wachache toka Kihesa. Alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugalo katika miaka ya 70, alikuwa  na tabia ya kusoma sana na pale alipotaka kupumzika basi rafiki zake wakubwa walikuwa Edson Mwamwani, Anderson Mwanyato na Ahmed Wanguvu wakitumia muda wao kucheza Bumping kwa wimbo wa Kung Fu Fighting, hapo ni mpaka jasho liwatoke.

MATAYARISHO YA SIKU YA WANAKIHESA YAPAMBA MOTO

Katika kikao cha wanaKihesa cha kutayarisha siku ya wanakihesa tarehe 2/12/2012, wanaKihesa waliokusanyika siku hiyo waliweza kukusanya shilingi laki saba cash. Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuwa kikao kijacho  cha tarehe 4/11/2012 kuwa ni muhimu sana watu wengi kufika kwani ndicho kitatoa picha kamili ya maandalizi ya ya tamasha.
 Pia tarehe 22/10/2012 matangazo ya tamasha yata anza kurushwa hewani rasmi na vituo vya Country Fm Iringa, na siku chache baadae vituo vya Clouds na Radio Free Africa vitaanza kutangaza taarifa za tamasha hilo.

SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO na ANDERSON ZABRON MWANYATO


 SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO ni mwana Kihesa  ambaye pia ni mkurugenzi wa MAJEMBE AUCTION MART ni mtoto wa kwanza wa mmoja wa wazee waanzilishi wa kihesa  Methusela Mwamotto .
 Setti ameajiri vijana, wazee na wakina mama wengi kutoka Kihesa kwenye kampuni yake ya Majembe. Setti amekuwa akijitolea kujenga na kukarabati makanisa, misikiti na kuwasaidia kwa matibabu, misiba , na kadhalika ya watu wengi wa Iringa.
    
  ANDERSON  ZABRON MWANYATO, mwanafunzi wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ndugu Philip Mangula ni msomi wa darasa la 7 tu. lakini mambo aliyoyafanya enzi za uhahi wake ni kama mtu mwenye PHD. Anderson Mwanyato ni mtoto wa 4 wa mama Sekinyunyu na Mzee Z.K Mwanyato.
 Ndiye alikuwa mkurugenzi wa Comfort Enterprises
ambayo inamiliki hotel ya Comfort Kitonga, akishirikiana na ndugu zake wawili hayati Joshua na Alex. Alitoa mchango mkubwa wa kijamii mkoani Iringa
 Mdogo wake Robert anasema anamkumbuka kwa kuwa mtu wa kuweza kushaurika, kwani yeye ndiye aliyemshauri ujenzi ule wa hotel porini  Wanamuziki Hayati Ndala Kasheba na King kiki ndio waliosindikizana na Robert ili kupiga katika uzinduzi wa hoteli ile 1993. Comfort hotel ipo chini ya mkurugenzi pekee  aliyebaki hai, Alex Zabron Mwanyato.

Tuesday, October 16, 2012

WAJUE WAZEE WA KIHESA 6


MZEE ERNEST MWANDANZI 
 Mzee huyu Mhehe wa Mufindi aliyestaafu uaskari akiwa na cheo cha Inspekta, ni mmoja wa wanzilishi wa Kihesa, alifanikiwa kuwa moja ya madiwani wa eneo hili.  Mzee Ndanzi ndiye baba mzazi wa Gerald Ndanzi wa Majembe Auction Mart.

MZEE MARTIN MLOWE 
 Mzee huyu Mbena  wa Kifanya - Njombe  ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa. Pamoja na kujishughulisha na kilimo eneo la Mangao Ismani, aliku.wa na bucha  pale Kihesa alibarikiwa kupata watoto wengi kama Gaspar, Oscar, Gerard, mtoto wa mwisho wa kiume Afred Mlowe alikuwa mchezaji kiungo wa Kihesa Stars, mchezaji mwenzie Robert Nyato hudai kuwa anamfananisha na Steven Gerald Alfred ndiye mtunza hazina wa Umoja wa wana Kihesa. Kwa sasa ni mfanyakazi wa Manispaa ya kinondoni 

Leo tutazungumzia wasifu wa wazee wa kihesa ambao ni wazazi wa ndugu Faustini Mdesa cosmas na tutamzungumzia Mzee wa kijana mhamasishaji wa siku ya wana kihesa  Ali mduba.

MZEE COSMAS MDESA
 Mzee huyu Mhehe wa Ifunda ni mwana Kihesa ambaye alijishughulisha na kilimo huko Kihologota Ismani akiwa na mjomba wake mzee Mwang’ingo. Mzee huyu ndiye baba mzazi wa mwenyekiti wa maandalizi ya siku ya wana kihesa Ndugu Faustine Cosmas Mdesa

MZEE JIMMY MWAMBAGO
 Mzee huyu Mbena wa Njombe ambaye alitinga Kihesa 1962, akitokea Tanga ambako alikuwa akifanya kazi upimaji na ramani. Mzee Jimmy alijiunga na kufanya kazi TANCUT na kusaafu mwishoni mwaka 1979. Bingwa huyu ambaye ni mzazi wa mwenyekiti wa Mkusanyiko wa wana Kihesa wa dar es Salaam Ndugu Nordrick Mwambago. Kwa sasa mzee Mwambago bado yupo anaishi Kihesa nyumbani kwake. Mwanae  Nodrick Jimmy Mwambago ndie  mwenyekiti wa wana KIHESA na mwenyekiti wa  kamati ya maandalizi ya siku ya wana Kihesa 2/12/2012

KABATI KATIBA STAR SEARCH YAPATA 20 BORA

Jumamosi tarehe 13 Oktoba katika ukumbi wa Welfare Center, mambo makubwa mawili yalifanyika, kwanza vijana wengi walioshiriki na wale waliokuja kufuatia Kabati Katiba Star Search walipata elimu nzuri ya Katiba ya Tanzania. Na pili ilikuwa burudani kwa kwenda mbele kutoka kwa vijana walioshiriki Star Search kuonyesha vipaji vyao. Vijana 150 waliweza kujitokeza kuonekana mbele ya jopo la majaji
majaji  Eddo Bashir (Ebony Fm), Temmy Mahondo (Country Fm), Dj Ammy Yeyo (Country Fm ), Agnes Anderson (Ebony Fm) na Dj Muba wa (Ebony Fm) . Mchujo uiofanyika baada ya hapo uliwezesha vijana 20 kuingia katika Top Twenty ya mpambano huo. Tarehe 27 Oktoba ndipo itakapoingia awamu ya pili ya shindano hili na Top Ten kupatikana.

Friday, October 12, 2012

TEMBELEA KIHESA KWA PICHA 2JOHN BAKERY(RIP), MWAMBA, KITIME


WAZEE WA KIHESA-5-MZEE RUBENI NYALUSI

Klerruu
Mzee huyu Mbena wa Lupembe alikuwa fundi stadi wa ujenzi na kuongoza umoja wa wajenzi Kihesa yeye akiwa mwenyekiti. Mzee huyu pia alijishughulisha na kilimo sehemu za Ngano Ismani, sambamba na Mzee Philipo Sawani. Hayati Mzee Nyalusi ndiye baba mzazi wa mchezaji mahiri wa ile timu maarufu Kihesa Stars Simoni Nyalusi.
Mchezaji huyu aliyekuwa na vituko vingi uwanjani, mpaka hivi leo bado yupo Kihesa akijishughulisha na ufundi ujenzi. Miongoni mwa vituko ambavyo mtoa habari hii Bwana Robert Nyato anasema hatasahau ni kitendo cha kupewa kadi nyekundu na refarii baada ya kumvuta pua mshika kibendera marehemu Bruda Modestus katika mechi kati ya Kihesa Stars na Lipuli zote za Iringa, refa  Mzee Maselenge alimtoa nje. Kituko kingine ni akiwa kama mtazamaji kwenye mashindano ya vyuo pale Kleruu aliingia uwanjani na kuifungia bao timu ya Kleruu na kusababisha mchezo kusimama takribani dakika 20 na wachezaji wa  timu ile ya Chuo cha Mbeya kuanza kumfukuza Simoni bila mafanikio yoyote.

TEMBELEA KIHESA KWA PICHA 1

Kama uliwahi kuwa mkazi wa Kihesa picha hizi zitakukumbusha mengi
WAZEE WA KIHESA-4-MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO

--> Mzee huyu Mbena wa Kidegembye alitinga kihesa 1935. kwa miaka kadhaa aliishi nyuma ya mlima Mafifi kabla ya kuja kuwa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa.  Kabla hajajulikana kama mkulima stadi alikuwa fundi washi, ndipo baadae akajishughulisha na kilimo kupitia mashamba makubwa aliokuwa nayo maeneo ya Chamdindi na Kifuluto kule Isimani. 
Mzee huyu akiwa na mkewe  mama Sekinyunyu alifikia uwezo wa  kumiliki  magari na matrekta. Mtoto wake wa kwanza  alikuwa Waston maarufu kwa jina la Fwasi Kilega ambaye kwa sasa ni marehemu na wengine kama Matata(Mbinu), Geofrey, Manase, Yotema wapo bado Kihesa mpaka leo.

Thursday, October 11, 2012

KABATI KATIBA STAR SEARCH- KUZINDULIWA JUMAMOSI


 Katika kuhamasiisha vijana wa Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua  KABATI KATIBA STAR SEARCH.  Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha, na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.

Tuesday, October 9, 2012

MSIBA KIHESA CHRISTOPHER MMASI HATUNAE TENA

CHRISTOPHER MMASI KAKA WA PATRICIA MMASI AMEFARIKI USIKU HUU HUKO IRINGA. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMINA
KWA MICHANGO MBALIMBALI YA RAMBIRAMBI UNAWEZA KUTUMA KUPITIA SIMU NAMBA 0754591929-DEVOTA MSILU
TAARIFA ZIMELETWA NA ROBERT MWANYATO

INDONYA NGOMI KUMWANI TWIYANGALILE

Kwa kuwa wameweka kidhungu ngoja tuweke Kiswahili kwa kifupi, TAHADHARI YA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI, KATI YA 8TH OKTOBA NA 11 OKTOBA 2012. MAENEO HUSIKA NI MIKOA YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, PWANI, NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA. KUNAWEZEKANA KUWEKO NA MVUA KUBWA YA KATI YA 50mm na 100mm KATIKA KIPINDI CHA MASAA 24,

Monday, October 8, 2012

WAZEE WA KIHESA 3- MZEE LOTTI LUPEMBE

-->   Mzee huyu wa kabila la Kibena alikuwa mkulima wa kawaida sehemu za Isimani kama ilivyokuwa kawaida  ya wazee wengi waanzilishi wa Kihesa. Baada ya mavuno mazuri walijenga nyumba zao  Kihesa. Mzee lotti alijizolea umaarufu  Kihesa kwa tabia yake ya kujitolea kupita asubuhi na mapema karibu kila mtaa na kutoa matangazo kwa wananchi , kwa mfano mtoto kapotea, ama kuna msiba umetokea n.k, kutokana na umaarufu huo wa Mzee Lotti, pale kihesa kuna mtaa unaitwa kwa LOTTI LUPEMBE .

Sunday, October 7, 2012

WAZEE WA KIHESA -2-MZEE ISAYA KIGAHE

MFARANYAKI CLUB
Mzee huyu wa kabila la Kibena ambaye mpaka leo yupo pale Kihesa, ni mmoja ya wazee waliofika eneo la Kihesa miaka ya 1940. Ukiachaa mwanae wa kwanza Gerald Isaya Kigahe ambaye amefariki miezi michache iliyopita, Mzee huyu alikuwa na mwanae  aliyeitwa Naftari Isaya Kigahe aliyefariki takribani miongo miwili iliyopita. Naftari  alikuwa JEMBE kwa wana kihesa, huyu bwana ndio mmoja wa wawaanzilishi wa lile eneo la Mkimbizi ki ujenzi na likaitwa kwa Kigahe. Moja ya vitu ambavyo vilimgalimu Naftari kuanza kukaa eneo hili ni kuvamiwa na majambazi na kupigwa risasi, aliuguwa na kupona majeraha na kuendelea na shughuli zake kama kawaida. 
Naftari Kigahe ndiye mwenye watoto akiwemo Rogers, Christina, Ganma na mkewe se Msamba maarufu Mama Kigahe bado yupo, Mkimbizi kwa Kigahe anaendesha biashara zake. Kwa waliosoma shule ya msingi ya Chemchem , miaka hiyo ikiitwa Consolata Primary school watamkumbuka Naftari kuwa alikuwa ndiye alikuwa mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule miaka hiyo. Bendi iliyokuwa chini ya Mwalimu Daudi Luhanga.

MBUNGE WA ZAMANI WA MUFINDI AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia muda si mrefu ni kuwa Mbunge wa zamani wa  Jimbo la Mufindi  kusini, Mhe.Benito Malangalila amefariki dunia  jana katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga mkoani  Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina.

WAZEE WA KIHESA -1-MZEE PHILIPO SAWANI

Mzee huyu wa kabila la Kikinga ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa alikuwa mkulima eneo la Ngano Isimani. Huku akiendesha biashara ya duka na bar hapo KIHESA katika nyumba yake ya kisasa kabisa. Wazee matajiri wa mji wa Iringa mfano Mzee Mwaitebele, Mzee Idd Mwangubi, Mzee Zabron Mwanyato pamoja na wafanya kazi maofisa kama Mzee Asam Sajio Kaduma walipenda kunywa kwenye bar ya Mzee Sawani. Lakini pia alipokuwa Mwenyekiti wa Tanganyika African Parents Association (TAPA) wa wilaya na alinunua jengo kwa pesa zake na kulifanya shule ya TAPA ambayo kwa sasa inaitwa Shule ya Msingi Mtwivila. Na mwalimu wa shule hiyo wa kwanza alikuwa Mwalimu Edward Chaula ( Baba Kichupa ) na Joseph Msandi ambao mishahara yao ililipwa na mzee Philipo Sawani. Jully Sawani ni mtoto wa Mzee Sawani ambaye alikuwa diwani wa kwanza Kihesa. Mzee Sawani alikuwa  mtu nadhifu sana akipendelea kuvaa English suit. Ama kwa hakika Mzee Philipo Sawani ana mambo mengi sana aliyochangia kwa Kihesa na maisha ya wengi tukisema tuyaandike yote hapatoshi.

Friday, October 5, 2012

WANAKIHESA WAONGEZEA MAJINA YA WAANZILISHI WA KIHESA

-->

Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa waongezwe hawa:

1.   Mzee Mtwivila,
2.     Fabian,
3.    Bibi Semtema,
4.    Mzee Lwaho,
5.     Victo Mwibalama,
6.     Mzee Mwambua (Baba Mussa),
7.     Mzee Ally Ngimba,
8.    Edward Wissa,
9.    Mgeni (Baba Jenifa),
10.                Kavilwa (Mourise),
11.                Msigomba,
12.               Balama (Baba Vero),
13.                Balama (mnyakilabu),
14.                Kibassa (Baba John),
15.               King Miking Kibassa (Babu yangu),
16.                Mzee Ng'owo,
17.                Ngogo (Mwanji),
18.               Tenga's wote (kuanzia Ngimonyi hadi wengine),
19.                Kalinga (Baba Moses),
20.               Nyalusi (Baba Mercy wa Timber),
21.                Mgeni (MZALENDO),
22.               Kigahe,
23.               G.G. Shambe,
24.               John Mbegalo,
25.               Gwegime (watoto wake hadi leo machampion),
26.                Sambala (Baba Marcelino),
27.               Mzee Luhanga (Baba yake Mwanyenza),
28.               Mzee Cheka (Baba ya Cheka Club Semtema),
29.                Mzee Gohage (Babu Fredy),
30.               Mzee James (Baba Baldo),
31.                Mwanzo Mgumu (Chao),
32.                Abel Lulandala (Baba Aidan),
33.                Fivawo,
34.               Mzee Kisonga.
 Pia orodha bado ni ndefu sana TUSAIDIANE KUIBORESHA

ENDELEA KUIJUA HISTORIA YA KIHESA

 WASIFU WA WAZEE WAANZILISHI WA KIHESA

 (1) MZEE JUMBE OMARY  
  Huyu mzee makazi yake ya mwanzo yalikuwa Kigonzile, baadae aliamia Kihesa karibu na mlima lilipo  kanisa la Kilutheli la Kihesa. alichaguliwa kuwa JUMBE,
Kazi yake aliamua kesi mbalimbali na kuwahamisha watu kuja eneo ilipo Kihesa kutoka  milimani, kwa mfano mlima Mafifi.
Kesi zilizo mshinda alizipeleka Kalenga wakati huo ndiko kulikwepo mahakama ya mwanzo. Mwandishi wa habari hii alimuona Mzee JUMBE OMARY mara ya mwisho mwishoni mwa miaka ya 1970. Alikuwa na ngeu usoni ambayo inasemekana  aliwahi kupigana na simba.

(2) AZIZA SEMGENI
 
 Bibi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa, yeye alikuwa anatibu kwa miti shamba, Eneo lake ndipo palipo jegwa shule ya msingi Kihesa. Wajukuu wa Bibi Aziza ni Mzee Jonas Mgeni ( Baba Zacho) Mzee Lwinusu Mgeni (Baba Riziki)

(3) SEMTEMA KUUKINGA
Mama huyu wa kabila la Kikinga aiifariki miaka michache aliopita ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa na alikuwa anamiliki eneo ambalo mpaka leo maarufu kwa jina la SEMTEMA  karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Tumaini

(4) SALUMU SOSOVELE
Huyu mzee kwa waliobahatika kumuona alikuwa pandikizi la mtu. mwenye kuongea kwa tabasamu. Baba yake mzazi ndie aliyemiliki eneo kilipo jegwa Chuo Cha Elimu Kleruu.Na kaburi la baba wa Salum lipo jirani na Kanisa Katoliki Kihesa.

Wednesday, October 3, 2012

WAZEE MAARUFU WALIOIJENGA KIHESA
-->
 1. MZEE JUMBE OMARY
 2. MZEE LOTTI LUPEMBE
 3. MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO
 4. MZEE PHOLIPO SAWANI
 5. MZEE RUBEN NYARUSI
 6. MZEE ANDREW MKOCHA
 7. MZEE METUSALA SINZIA MWAMOTTO
 8. MZEE NIKOLAI CHAWE
 9. MZEE PESAMBILI RAIS
 10. MZEE JUMANNE MWANDAMIZI
 11. MZEE JIMMY MWAMBAGO
 12. MZEE CAPRO MAHANJAM MDEGELA
 13. MZEE JOHN MAUYA
 14. MZEE FEDRICK KIHADE
 15. MZEE SHEM MAINGARA
 16. MZEE VICENT MSEMWA MFARANYAKI
 17. MZEE LUBAFU LWASOMBA
 18. MZEE ELEUTEL KIMILIKE
 19. MZEE RUPI SABA MKUSA
 20. MZEE GARUS KING'UNZA
 21. MZEE GARUS MWANYAKUNGA
 22. MZEE JAMES CHOMI
 23. MZEE WILLIAM MNG'ONG'O
 24. MZEE MATHAYO MNG'ONG'O
 25. MZEE METUSALA MNG'ONG'O
 26. MZEE PETER MSILU
 27. MZEE EDWARD MMASI
 28. MZEE GEORGE SAWALA
 29. MZEE LUCAS MKUSA
 30. MZEE MUSSA MWACHANG'A
 31. MZEE AUGUSTINO MWACHANG'A
 32. MZEE EMMANUEL MWACHANG'A
 33. MZEE MARTIN MLOWE
 34. MZEE JOHN NZALI BALANCE
 35. MZEE MKINGA SAFI MBILINYI
 36. MZEE AMOSI MPOGOLE
 37. MZEE SAID KITENGE
 38. SHEKHE MDOKA MAULID
 39. SHEKHE SAID KALELA
 40. SHEKHE SAID WANGUVU
 41. MAMA DIANA MAGRETH
 42. MZEE MPOGOLE (BABA SAREHE)
 43. MZEE ALEX SANGA
 44. MZEE ISAYA KAGAHE
 45. MZEE SAMSON NYATO
 46. MZEE SAMWEL KINYUNYU
 47. MZEE MALIO  MSILU
 48. MZEE HAMISI KINGENG'ENA
 49. MZEE NGAIRO( BABA STIVIN)
 50. MZEE KUDINGWA MAPUNDA
 51. MZEE FRANSIS KITIME
 52. MZEE LAMEKI TUMBUKA
 53. MZEE IBRAHIM MWIBARAMA
 54. MZEE KALYIEMBE ( BABA ANYWELWISE)
 55. MZEE SIXMUND MOLAMOLA
 56. MZEE JOSEPH KASUMRI SANGA
 57. MZEE  MKULU EZEKIA
 58. MZEE  CHODOTA (BABA ELIABI)
 59. MZEE MTEVELA (BABA FOIDA)
 60. MZEE OBADIA NGOGO
 61. MZEE PETER NGWIVAHA
 62. MZEE EDWARD MAKWETA
 63. MZEE ADAMU KAPUNGU
 64. MZEE ELIEZA MNG'ONG'O
 65. MZEE EDSON MWAMWANI
 66. MZEE JOHN LUSUNDE
 67. MZEE ZABRON KINYAMAGOHA
 68. MZEE EPHRANI KILATU
 69. MZEE SALUM NYENZI
 70. MZEE ADAM SAJIO KADUMA
 71. MZEE JONASI MGENI
 72. MZEE ZAKARIA CHUWA
 73. MZEE MAIGE MACHIBYA
 74. MZEE KUFAKUNOGA MAHAMODU
 75. MZEE PETER LUPEMBE
 76. MZEE LINGWENDU SANGA
 77. MZEE JOHN KANYWENDA 
 78. MZEE MARTINE MWAMBILINGE
 79. MZEE AMRAN MDEMU
 80. MZEE HENRY NYANYEMBE
 81. MZEE JOHN LUHANGA
 82. ZABRONI LUVINGA
 83. MZEE ALI MDUBA
 84. MZEE MARKO MFUGALE
 85. MZEE ALFREDY MBATA
 86. MZEE JOHN GILIKI
 87. MZEE JOHN EJO
 88. MZEE GALAHENGA BEATUSI
 89. MZEE MDENDEMI
 90. MZEE MWANYWAEGE
 91. MZEE DANIEL LUGENGE
 92. MZEE KIDUNU
 93. MZEE MNG'ONGO'
 94. MZEE MBILINYI
 95. MZEE MWANANGUNULE
 96. MZEE KANDANDA
 97. MZEE TITIKOO
 98. MZEE SALUM MDEGIPARA
 99. MZEE FUNGO
 100. MZEE MGOMBELE
 101. MZEE NZELU
 102. MZEE KIDULILE
 103. MZEE MBIFILE
 104. MZEE ELIAS SANGA
 105. MZEE NGWALE
 106. MZEE  MARTIN KIDUKO
 107. MZEE KIWELE
 108. MZEE MWITA
 109. MAMA GIFT
 110.  MZEE NGALAWA (BABA MWAMBA)
 111. MZEE DICKS DISUZA
 112. MZEE MAGAVA
 113. MZEE FARAHANI
 114. MZEE BENARD MBIGILI
 115. MZEE POYO
 116. MZEE MNYAMWANI
 117. MZEE KAPANDE
 118. MZEE MWALIWELO
 119. MZEE MALILA
 120. MZEE CHENGULA
 121. MZEE FURAHISHA
 122. MZEE  WILILO (BABA ROBERT)
 123. MZEE MASENYA
 124. MZEE BABA HILDA
 125. MZEE MASHAKA WILLBAKI
 126. MZEE KIKOSI JUMA MASOUD
 127. MZEE COSMAS MDESA
 128. MZEE MLIMBILA
 129. MZEE MBOMBWE
 130. MZEE SOSTEN KYANDO
 131. MZEE NDITI 
 132. MZEE BABA MAYASA
 133. MZEE WEEK END
 134. MZEE LUGENGE
 135. MZEE LUGALA
 136. MZEE MWANG'INGO
 137. MZEE ODO
 138. MZEE RUNYASI
 139. MZEE SEKAHANGA
 140. MZEE MFIKWA
 141. MZEE AMBROS MWANGWADA
 142. MZEE KIWONAOMELA
 143. MAMA SAMAMBA
 144. MZEE LUCHABIKO KAPUGI
 145. MCHUGAJI CHUSI
 146.  MZEE MACHILINA
 147. MAMA SEMPOGOLE
 148. MAMA GEORGE KUMBEMBA  MWAKIMBENGONDO MGODAGWIVAHA MUNYIDUNDA
 149. MZEE SAMUEL BWANANGONDO M.M MWAKIMBE
                                                         
                               
NB: KUNA WAZEE WASIOPUNGUA 200 WALIO IJENGA KIHESA TUTAENDELEE KUSAIDIANA KUWAKUMBUKA KAMA MAJINA YAO HAYAPO HAPA
                                    KATIKA MAANDALIZI YA SIKU YA WANA KIHESA TUTAKUWA TUNAWACHAMBUA WASIFU WA WAZEE HAWA.
                                IMETAYARISHWA NA ROBERT MWANYATO: MRATIBU WA TAMASHA LA WANA KIHESA