Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Thursday, October 11, 2012

KABATI KATIBA STAR SEARCH- KUZINDULIWA JUMAMOSI


 Katika kuhamasiisha vijana wa Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua  KABATI KATIBA STAR SEARCH.  Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha, na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.

No comments:

Post a Comment