Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Friday, October 12, 2012

WAZEE WA KIHESA-4-MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO

--> Mzee huyu Mbena wa Kidegembye alitinga kihesa 1935. kwa miaka kadhaa aliishi nyuma ya mlima Mafifi kabla ya kuja kuwa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa.  Kabla hajajulikana kama mkulima stadi alikuwa fundi washi, ndipo baadae akajishughulisha na kilimo kupitia mashamba makubwa aliokuwa nayo maeneo ya Chamdindi na Kifuluto kule Isimani. 
Mzee huyu akiwa na mkewe  mama Sekinyunyu alifikia uwezo wa  kumiliki  magari na matrekta. Mtoto wake wa kwanza  alikuwa Waston maarufu kwa jina la Fwasi Kilega ambaye kwa sasa ni marehemu na wengine kama Matata(Mbinu), Geofrey, Manase, Yotema wapo bado Kihesa mpaka leo.

No comments:

Post a Comment