Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, September 30, 2012

KIKAO CHA WANAKIHESA CHAFANA

Kikao cha wanaKihesa kilichofanyika KGB Hotel Jumapili hii tarehe 30 September, kilifana kwa ongezeko kubwa la washiriki wa kikao hicho. Pamoja na mengine, kwa sasa lengo kubwa ni kuwa na Tamasha la Wana Kihesa tarehe 2 Desemba 2012, ambalo limepangwa kuwepo katika eneo la Kijiji cha Makumbuso.  Baadhi ya wanaKihesa walioonekana katika kikao cha safari hii ni pamoja na Mikidadi Mwachang'a ambae alisema wazi na kwa uchungu kuwa alikuwa anaombea uwepo wa umoja wa namna hii miaka mingi. Mwana kihesa mwingine alikuwa ni mwana Kihesa maarufu Fredrick Mwakalebela ambae nae pia aliahidi kuwa bega kwa bega katika kufanikisha umoja huu. Fedha taslimu shilingi  Laki 6 na nusu zilichangwa na ahadi za milioni moja zilitolewa. Mkutano ujao utakuwa tarehe 14 Oktoba katika ukumbi huohuo wa KGB Hotel, Ubungo Riverside

Thursday, September 20, 2012

KWA WALIOSOMA SHABAHA KATI YA 1971

Robert Nyato alijiunga na shule ya msingi ya Shabaha, ambayo awali ilikuwa ikiitwa Aga Khan Primary School. Jina la Shabaha lilitokana na kuwa, nyuma tu ya shule , pale mbele ya nyumba za Mzee Poyo palikuwa na sehemu ambayo askari wa FFU walikuwa wakitumia katika kujifunza kulenga shabaha, watoto waliokuweko wakati huo watakumbuka kuwa mara baada ya mazoezi ya shabaha watoto walikuwa wakienda kuokota maganda ya risasi yaliyotumika. Mkuu wa shule hii wakati huo alikuwa Mwalimu Chungu, Robert alikuwa na rafiki yake Evaristo Kimile. Walimu waliokuweko wakati huo walikuwa Mwalim Mama Mbaruku ambaye ndiye alikuwa mwalimu wa darasa la kwanza, Mwalimu Kitojo akiwa mwalimu wa nidhamu. Hatimae alifikia kuingia shule ya Highlands alipokutana na rula za mwalimu mkuu mwalim Sheikh, akisindikizwa na mwalimu Chalamila,Mwalimu Mwambeta,, Shawala, Mwal Mayagila, Mama Masima, Mwal Mpete, na Mwakalinga ilikuwa ni listi tosha ya kuhakikisha akina Mohamed Siaga, Ally Sareva, Maneno Ndanzi na Robert Kipandule Nyato wanasoma ipasavyo.....una kumbukumbu za enzi zako? zitume kwa sms 0713274747 au jkitime@gmail.com zitundikwe kwenye blog hii ASANDE

MKUTANO WA WANAKIHESA 30 SEPTEMBER 2012 KGB HOTEL

 Mratibu wa WanaKihesa Robert Kipandule Mwanyato anawaomba wana Kihesa kuhudhuria kwa wingi kikao muhimu tarehe 30 September 2012, katika ukumbi wa Hoteli ya KGB iliyopo Riverside Ubungo. Pia angependa kuwataarifu wote kuwa viongozi wa liochaguliwa katika kikao cha terehe 9 September 2012 ni kama wafuatao;
Mlezi-Sethi Motto
Mwenyekiti-Nordrick J Mbago
Makamu Mwenyekiti- Richard Mkocha
Katibu -Bright Robert Nyato
Katibu Msaidizi-Devota Peter Msilu
Mtunza Hazina Alfred Mlowe
TUNAOMBA TUHUDHIRIE MKUTANO HUO KWA WINGI

Sunday, September 16, 2012

WANAKIHESA WA DAR ES SALAAM, WAKUTANA KUPANGA MAMBO YAO

Mkutano wa pili WanaKihesa ulifanyika leo katika hotel ya KBG maeneo ya Riverside Ubungo. Nia ya mkusanyiko huu ni kuangalia namna ya WanaKihesa kuweza kukutana na kushirikiana katika mambo yao ya pamoja. Tarehe 2 Dec 2012 ni siku ambayo imekubalika kuwa siku ya WanaKihesa, hivyo kutakuwa na shughulimbalimbali zitakazofanyika siku hiyoikiwemo chakula cha pamoja vinywaji, na michezo mbalimbali ikiwemo muziki wa bendi hasa Tancut.MKutano ujao tarehe 30 September 2012