Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, September 30, 2012

KIKAO CHA WANAKIHESA CHAFANA

Kikao cha wanaKihesa kilichofanyika KGB Hotel Jumapili hii tarehe 30 September, kilifana kwa ongezeko kubwa la washiriki wa kikao hicho. Pamoja na mengine, kwa sasa lengo kubwa ni kuwa na Tamasha la Wana Kihesa tarehe 2 Desemba 2012, ambalo limepangwa kuwepo katika eneo la Kijiji cha Makumbuso.  Baadhi ya wanaKihesa walioonekana katika kikao cha safari hii ni pamoja na Mikidadi Mwachang'a ambae alisema wazi na kwa uchungu kuwa alikuwa anaombea uwepo wa umoja wa namna hii miaka mingi. Mwana kihesa mwingine alikuwa ni mwana Kihesa maarufu Fredrick Mwakalebela ambae nae pia aliahidi kuwa bega kwa bega katika kufanikisha umoja huu. Fedha taslimu shilingi  Laki 6 na nusu zilichangwa na ahadi za milioni moja zilitolewa. Mkutano ujao utakuwa tarehe 14 Oktoba katika ukumbi huohuo wa KGB Hotel, Ubungo Riverside

No comments:

Post a Comment