Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, November 18, 2012

WANAKIHESA WACHANGA ZAIDI YA MILIONI MBILI

Kikao cha matayarisho ya siku ya Wanakihesa 2/12/2012, inayotegemewa kufanyika Makumbusho Dar es Salaam kimekuwa cha mafanikio makubwa kwa wajumbe kuwa wengi zaidi, wajumbe wamezidi kufanikisha michango yao,na kuwa mpaka sasa zimekusanywa zaidi ya shilingi milioni mbili na nusu. Leo tena  kikao kilichangamka sana kikiwa na wajumbe wengi zaidi akiwemo Brown Mbigili, ambaye aliburudisha kikao kwa kutukumbusha Rais wa Kihesa…Mtambule marehemu Mzee Mbigili. Picha za kikaoSaturday, November 17, 2012

MHE. JACKSON MAKWETA AFARIKI DUNIA


MZEE Jackson Mvangila Makweta, Mbunge wa Njombe wa muda mrefu (1975-2000), na Mzee aliyewahi kushika nafasi ya kadhaa za Uwaziri katika serikali ya Tanzania amefariki jioni hii katika hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya Moyo Mungu Amlaze pema peponi Amen

Thursday, November 15, 2012

Wednesday, November 14, 2012

18/11/2012 SIKU YA MKUTANO MUHIMU KWA WANAKIHESA

MwanaKihesa Mage
Jumapili tarehe 18/11 kuna kikao muhimu kwa Wanakihesa, Wanakihesa wote mnakaribishwa kwenye kikao hiki cha maandalizi. kama kawaida kikao kitakuwa KGB Hotel Riverside kuanzia saa 9 mchana, tutangaziane.
Matangazo ya sherehe yetu ya mwezi Desemba yataanza katika Clouds Radio wiki hii, na yaendelea hadi kilele cha  siku muhimu ya siku ya Wanakihesa mwanzoni mwa Desemba.

Sunday, November 11, 2012

MSIBA MWINGINE KIHESA

MwanaKihesa Ahmed Wanguvu amefiwa na mama yake mchana wa tarehe 11/11/2012 Kihesa Iringa. Mazishi yatakuwa tarehe 12/11/2012. Kwa kutoa salamu za rambirambi unaweza kutumia namba za Ahmed 0754 319850 na 0767 290300.
Mungu amlaze mama yetu pema peponi

Wednesday, November 7, 2012

PICHA YA WIKI--WANAKIHESA

Hii ilikuwa mwaka 1989 TANCUT HALL mbele ni Robert K Mwanyato na nyuma yake ni  DC wa Kibonda Mr Venance Sethi Mwamoto kumbukumbu safiii

Sunday, November 4, 2012

KIKAO CHA WANAKIHESA CHAFANA

Jana tarehe 4 Novemba 2012, kulifanyika  kikao kingine cha WanaKihesa, Katika hali ambayo inaonekana jambo la kukusanyika kwa Wana Kihesa ni jambo zuri mkutano wa jana ulikuwa na washiriki wengi kuliko mikutano ya awali, jambo ambalo ni jambo zuri sana kwani uzoefu unaonyesha kuwa mikutano ya aina hii huanza na watu wengi kisha wakapungua kila kikao na hatimae kufa kabisa kwa ushirikiano huo. Kamati mbalimbali zilizochaguliwa nazo zinaendelea vizuri kwani maandalizi ya Tamasha kubwa la WanaKihesa yamekwisha kamilika kwa asilimia 80. Kikao kijacho kimepangwa kuwa tarehe 18/11/2012.
 Moja ya mambo yaliyofurahisha katika kikao ni kuwepo kwa wajukuu wa Mzee Mfaranyaki Cilla na Kidunu, kweli mkusanyiko huu umekuwa wa furaha kubwa kwani kuna wengi wanaokutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi , wengine kukutana kwa mara ya kwanza toka walipokuwa watoto, ni furaha tu. Wadau mnakaribishwa katika kikao kijacho katika tarehe iliyotajwa, katika ukumbi wa hoteli ya KGB pale Riverside Ubungo.

Thursday, November 1, 2012

MZEE MBIGILI AFARIKI DUNIA LEO 1/11/2012 JIJINI DAR ES SALAAM

WAZEE WETU WOTE HAWA WAWILI SASA NI MAREHEMU. MZEE MBIGILI AKIWA KWENYE KOTI JEUSI NA PADRI MWOGOFI. MZEE MBIGILI AMEFARIKI LEO  1/11/2012 SAA NNE ASUBUHI JIJINI DAR ES SALAAM. TARATIBU ZINAFANYIKA ILI KUWEZA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KWENDA IRINGA KESHO.
MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI AMEN