Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, November 4, 2012

KIKAO CHA WANAKIHESA CHAFANA

Jana tarehe 4 Novemba 2012, kulifanyika  kikao kingine cha WanaKihesa, Katika hali ambayo inaonekana jambo la kukusanyika kwa Wana Kihesa ni jambo zuri mkutano wa jana ulikuwa na washiriki wengi kuliko mikutano ya awali, jambo ambalo ni jambo zuri sana kwani uzoefu unaonyesha kuwa mikutano ya aina hii huanza na watu wengi kisha wakapungua kila kikao na hatimae kufa kabisa kwa ushirikiano huo. Kamati mbalimbali zilizochaguliwa nazo zinaendelea vizuri kwani maandalizi ya Tamasha kubwa la WanaKihesa yamekwisha kamilika kwa asilimia 80. Kikao kijacho kimepangwa kuwa tarehe 18/11/2012.
 Moja ya mambo yaliyofurahisha katika kikao ni kuwepo kwa wajukuu wa Mzee Mfaranyaki Cilla na Kidunu, kweli mkusanyiko huu umekuwa wa furaha kubwa kwani kuna wengi wanaokutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi , wengine kukutana kwa mara ya kwanza toka walipokuwa watoto, ni furaha tu. Wadau mnakaribishwa katika kikao kijacho katika tarehe iliyotajwa, katika ukumbi wa hoteli ya KGB pale Riverside Ubungo.

No comments:

Post a Comment