Pages

Sunday, July 31, 2022

UNAJUA KUWA ZAMANI MHEHE MWANAUME AKIFA ANAZIKWA NA MKEWE ALIYE HAI?


 

Kama nilivyoeleza katika makala zilizopita, wale  watu weupe waliowatimua Wategeta walikuwa pia wakifanya biashara ya kuuza watumwa. Koo nyingi za Kihehe hazikukubali kuuuzwa hivyo wengine waliona heri wauwawe, wengine waligoma kula hivyo kufa wakiwa katika masafara wa kuelekea pwani, na wengine walikimbia mbali kutoka maeneo yao ya asili.
Tuliona jinsi kabila la  Wanyakyusa lilivyopatikana kutokana na kusambaratika huko. Wagogo pia ni kabila lilitokana na fujo hizo. Koo mbalimbali za Wahehe walikimbilia kaskazini na kufika mpaka sehemu inaitwa Mkofa kando ya mto Lyambangali,  wakawa wanatafuta namna ya kuvuka kwenda upande wa pili, sehemu moja wakakuta gogo kubwa limeanguka na kulala juu ya mto na kutengeneza aina ya daraja, hivyo wakaweza kuvuka kumkimbia adui, kwa kukumbuka kuvuka huko, wahehe wale walijiita Vanyagogo, jina ambalo baadae likafupishwa kuwa Wagogo.
Wagogo wengi kwa kukumbuka walikotoka huwaita Wahehe wajomba zao. 
Kuna simulizi za kale kuwa Warangi walitokana na watu watu weupe waliohamia Uheheni  kutoka Usambara.
Wakati ule koo kadhaa zilizokuwa zikiishi karibu na bahari ya Hindi zilijikuta zikiwa na machotara wengi wa Kiarabu na baadae waKireno. Watu hawa weupe toka Usambara walikuja kuishi sehemu ya Ugunda iliyokuwa ikiitwa Ilamba na wengine kuhamia Usagala.
 Kuna Wasagala wa zamani walikuwa weupe na wanaume wakawa na nywele nyingi mikononi na kifuani na walikuja kuwa na muitiko au mwidikiso wa Mnyakami, inawezekana walikuwa na  uhusiano na Wakami wa Ulugulu. Hawa watu weupe walienea  sehemu nyingi za Uhehe, Ubena na Ukimbu.  Wale waliobaki Ugunda, Wahehe walianza kuwaita Valangi. Valangi  hawa na ndugu zao Wanyiramba walikuja kuhamia maeneo ilipo Singida sasa. Kuna wakati wajukuu wa Valangi hawa waliamua kurudi kwao Uheheni, lakini karibu na Dodoma wakakutana na ukoo wa Wadongwe waliokuwa chini ya Kiongozi wao Muyovela, vita kali ikaanza  wakashindwa na wakalazimika kukimbilia ilipo Kondoa sasa na huko wakaishi na kuongezeka na kuwa kabila kubwa.
Makundi mengine ya watu weupe  yalisonga mbele mpaka Ukimbu,  kundi jingine likahamia sehemu za Ilembula, kundi jingine likahamia kwa muda sehemu za Wasa, kisha kuelekea Malangali.
Kundi hili ndilo linalosemekana liliingiza kilimo cha kulima mahala kwenye majani kwa kugeuza udongo na kutengeneza matuta kwa kufukia majani. Majani yale yaliachwa kwa muda ili yaoze na kisha ndipo mbegu hupandwa.
Kilimo hiki kilileta mazao mengi, killimo hiki kiliitwa Malongo, na sehemu ile ya malangali ikaitwa Ilongo.  
Wahehe huita mavuno mengi kuwa ni Sanga. Katika sehemu hiyo ya Ilongo kukaweko na kundi fulani la wakulima waliokuwa hodari wa kulima malongo na hivyo kuwa wanapata mavuno mengi wakaanza kuitwa Vanyasanga, mafanikio ya Vanyasanga yakwaletea maadui na wakaamua kuhamia sehemu za Ukinga na Uwanji, na ndio chanzo cha koo za Sanga huko Ukinga na Uwanji.
Ukoo wa Kihaule pia husema walitokea Ilongo, na hata mwitiko wa binti wa kina Kihaule ni Nyamalongo. Wazee wa Upangwa husema kina Kihaule wa kwanza kuingia huko walikuwa weupe na walileta kilimo cha malongo, pia ndio waliokuja kusitisha mila ya kumzika mke akiwa mzima mzima kama mumewe amefariki, mila hii hata Wahehe awali  walikuwa nayo. 

Saturday, July 30, 2022

WANYAKYUSA WALITOKA UHEHENI

 


Vanu velu au watu weupe waliotoka Kilwa waliingia nchi ya Uheheni kwa amani na wakaendelea kuishi kwa amani na hatimae kuwa sehemu ya wenyeji, mfano nilioutoa ni wakina Kiwhele. 

Lakini kuna kundi jingine la watu weupe hawa waliingia kutoka kaskazini na kuingia katika eneo lililoitwa Ugunda, wenyeji wa Ugunda walikuwa ni Wategeta, habari zao nilikwisha zizungumzia awali. Jina la Ugunda lilitokana na babu yao mmoja aliyeitwa Mugunda.  Eneno la Ugunda kwa sasa linaitwa Image na tutaelezana chanzo cha jina hilo baadae. Kama mnakumbuka, niliwaeleza kuwa Wategeta walikuwa wafua chuma wazuri sana na walikuwa watu walioishi kwa mpangilio mzuri katika kazi yao hiyo, pia niliwaambia kuwa walikuwa ni watu wenye maungo makubwa yenye afya hawakuwa watu wa mchezo. Kuna kundi moja la Wahumma kutokea aidha Pawaga au Izazi, liliwashambulia Wategeta hawa ili kuwanyang’anya ng’ombe. Pamoja na Wahuma kuwa na silaha za kutisha ,Wategeta waliwakamata adui zao hao kwa mikono  na kuanza kuwachanachana vipande. Walimbakiza Muhumba mmoja tu nae walikata masikio wakamwachia aende kwao akahadithie. Baada ya hapo Wategeta wakawa mara kwa mara wanawashambulia Wahuma na kuwanyang’anya ng’ombe bila upinzani mkubwa. 
 
Lakini hili kundi la watu weupe kutoka kaskazini liliwazidi sana nguvu Wategeta. Wenyeji wengi wakalazimika kukimbia nchi yao na kukimbilia upande wa iliko Pawaga sasa, wale maadui waliwafwata mpaka huko na kuwamaliza na waliobaki kuwachukua watumwa na kwenda kuwauza Pwani. Mahala palipokamilisha vita hiyo palikuja kuitwa Malikilo maana yake pa kumalizia. Siku hizi panaitwa Kidali.

Wategeta wengine walikimbia kaskazini na kufika mpaka ulipo sasa mpaka wa Kenya na Uganda. Huko wakalikuta kabila la Wasamia na kuwashinda na kuwa watawala wao. Hata siku hizi wajukuu zao hujiita Bahehe na kusema kuwa babu zao walitokea Uheheni. Kundi jingine la Wategeta lilikimbilia Mahenge na baadae kuanza kufuata bonde la  Kilombelo kisha kuingia Ubena na kuendelea na safari hadi Kaskazini mwa Ziwa Nyasa, wakaanza kuishi sehemu waliyoiita Kavala, maana yake  peupe penye kuwaka jua, wakaendelea na kazi yao ya asili ya uhunzi. Wengi wao walikuwa wa ukoo wa kina Chusi na wakawa watawala, jina lao likageuka kuwa Chusa,  Wagonde wakaligeuza jina hilo kuwa Wanyachusa, au Wanyakyusa. Kuna Wanyakyusa ambao hatimae walirudi Uheheni kwa mfano ukoo wa akina Kalinga, hawa walitumia majina kama Kwilengilyova, yaani maji yangurumayo, wakikumbuka  maporomoko ya maji katika sehemu walizopita wakati wakisafiri wakifuata bonde la Kilombelo. Wengine wakijiita Magalamatitu, wakikumbuka sehemu ambapo kulikuwa tambarare  ya  ndege wengi weusi ambayo ipo mpaka leo. Hawa watu weupe waliowafukuza Wategeta waliacha uzao wao katika nchi ya Usagala. Wajukuu hawa wa Wasagala wa zamani, ambao hujulikana kama Vanyikami, huwa na madai tofauti, wengine wakidai kuwa asili yao ni waarabu, wengine wakidai asili yao ni wazungu. Wanahistoria wengi huona hiyo si rahisi kwani wangekuwa Waarabu, lazima wangeanzisha dini ya Kiislamu na hali kadhalika wangekuwa wazungu kungeletwa pia ukristu. Kinachodhaniwa ni kuwa Vanu velu hawa walikuwa ni machotara au watu tu wenye ngozi angavu.

UNAJUA WAHEHE WALITOKEA WAPI 2 ? marekebisho

 


Wabena ndio chanzo cha Wahehe. Inasemekana jina la kabila hili lilitokana na kutofautiana katika mshangao na kabila lao mama la Wabena. Wahehe walikuwa wakishangaa kwa kusema He he, Wabena walikuwa wakishangaa kwa kusema khe khe. Baadaye Wahehe walitumia sauti hiyo hata wakati wakiwa vitani. Kama nilivyosema katika sehemu ya kwanza ya simulizi hii, makundi mawili ya wabena yaliondoka Nyumbanitu na kuelekea Kaskazini mashariki na kuja  kuishi kwa muda Magharibi mwa ilipo Malangali sasa.  Lakini tena kukaweko na mgawanyiko, kundi moja lilielekea  bonde la Lyambangali na kuanzisha  kabila la Wasangu , wakati kundi jingine likielekea upande wa pili na hili likaja kuwa chanzo cha Wahehe. Katika kugawanyika huku, sehemu waliyoanzia kugawanyika ikaitwa  Igawilo maana yake penye kugawa nchi. 

Kama ilivyokuwa katika tabia za Kibantu watu hawa waliokuja kuitwa Wahehe awali waligawanyika katika koo mbalimbali, japo inasemekana walikwisha anza kujitambulisha kama Wahehe.  Kati ya  koo  maarufu walikuweko  akina;  
Vigawilo – Hawa ni wale waliobaki pale Igawilo,   na baadae wengine wakaaza kusambaa katika bonde la Lyandembela na kuanza kuitwa Vilongo. Mwiko wao hawa ulikuwa bandama, jamaa wa ukoo huu ni akina Kibodya na Mugandu.
Vahafiwa – hawa walienea katika sehemu zinazoitwa siku hizi Tanangozi, welu, kalenga Ntsihi, na maeneo yanayozunguka mji wa Iringa.

Kuna wakati maeneo haya yalipata uhaba mkubwa wa mvua hivyo kukawa na njaa na hata watu wengi  wakafa kwa njaa, waliosalimika walikuja kupata mwidikiso wa  Vahafiwa maana yake waliofiwa na wengine walikuwa na mwidikiso wa Mponela yaani aliyepona njaa. 

Wengine walikuja kuitwa Vanyalugome kwa sababu ya desturi yao ya kutengeneza mitego ya wanyama kwa  kuchimba mahandaki.

Mwiko wao hawa ilikuwa ni nyopolwa, Yaani mimba ya mnyama yoyote.

Labda niseme hapa hapa kuwa mwiko maana yake hawaruhusiwi kamwe hata kuonja nyama hiyo.

Kati ya koo zinazojulikana kutoka kundi hili ni akina Mugovano, Mukemangwa na mutono,

Vanyandevelwa- maana yake wepesi kuchokozwa, makazi ya kundi hili yalikuwa kati ya barabara mbili zilizoanzia Iringa, yaani ile ya kwenda  Dar es Salaam na ile ya kwenda Dodoma

.Awali nao mwiko wao ulikuwa nyopolwa lakini walikuja kunyangwa nchi na kundi lililoitwa Vanyamahuvi na kuja kutawaliwa nao.

 Hawa Wanyamahuvi wakaja kutwaa jina la Vanyandevela lakini wakaendeleza mwiko wao ambao ni ndege kanga, Ni vigumu siku hizi kupambanua nani ni Mnyandevela wa awali na nani Mnyamahuvi wa awali

Vategeta hawa walikuwa na umuhimu sana katika kabila la wahehe kwani walikuwa mafundi wa kufua chuma.

Wategeta ndio waliounda mikuki, mundu shoka na kadhalika. Wategeta waliishi karibu na kila ukoo wa Wahehe na hasa sehemu zenye mchanga uliweza kutoa chuma, wengi walikuwa warefu wenye maungo yenye afya na hivyo basi waliweza kufikia kutawala katika sehemu nyingi walizokuwa wakiishi.

Wategeta waligawana kazi, walikuwa na sifa ya kuwa wana mipangilio katika maisha yao.  Wale waliokuwa mabingwa wakutafuta kuni kwa ajili ya mkaa wa kuyeyushia chuma waliitwa Vanyantsagala …nzagala ni kuni, baadae walikuja kufupishwa na kuitwa Wasagala.

 Wategeta ambao walikuwa na utaalamu wa kuchagua mchanga bora kwa chuma waliitwa Vayunga, ambao ndio chanzo cha Watsungwa. Kutokana  majina haya walipoenea na kuwa wengi sehemu waliyoenea Vayunga ikaitwa Utsungwa na walikoenea Wasagala ikaitwa Usagala.

 Mwiko wa Wategeta ni mato kwa Kiswahili mbawala na wengine mwiko wao ni dundulu yaani twiga. Inasemekana waliamini kuwa kwa kula nyama ya wanyama hao  wangepata ukoma ,kwani ngozi ya binadamu huwa na mabaka meupe kama twiga, kama ameambukizwa ukoma.

Kati ya koo za Wategeta maarufu ni Chusi na kina Mveyange

Wakilwa,,, hawa waliitwa hivi kwa kuwa walitokewa Kilwa na kuingia sehemu inayoitwa siku hizi Mufindi kwenye robo ya kwanza  ya karne ya 16. Yaani mwaka 1500. Hawa hawakutokana na Wabena kama Wahehe wengine.

Hawa walikuwa na ngozi ya maji ya kunde na walikuwa na nywele nyingi mikononi na kifuani.  Nywele ambazo Wahehe huziita Lyagi,hivyo Wakilwa pia wakaaitwa Vanyalyagi. Dalili hizi ziliwatofautisha na wabantu wengine. Inasemekana walipokuwa badi Kilwa, walichanganyika na Wareno na Washirazi waliokuwa tayari wametua Kilwa wakati huo.

Kati ya Wakilwa wa Uheheni ni akina Kihwele ambao walipoenea Uheheni walionyesha kutengeneza vifaa vya chuma bora kuliko Wategeta.  Huko Katanga Kongo kuna ukoo unaitwa Kiwele, na kuna uwezekano kuwa ni ndugu wa Kihwele wa Uheheni kwani wote walikuwa wakizika wafu wao kichwa kikielekea mashariki, kwa kukumbuka kwao  Kilwa, ambayo iko mashariki mwa Katanga na Uhehe pia,


NDONGWA SA KIHEHE -unaejua maana weka jina lako na maana kwenye comments

 



1. Muhwehwe luheko

2. Imbwa ndavila pasi ye nyisi.
3. Kwe wisagalila, ndemuyago ndaiwopola.

4. Ukwegi hanzu na malagala. (Mkwega mahanzu na malagala)

5. Umulomo si kitegulo

6. Umpafi si muwulasi

7. Chalonzile mkwamilingwada, alakiwene

8. Uwudodi waikala

9. Kinyawihanga, kinawigafi, ulihuvila nda

10. Ulanonela ing'wale, nonelage ulutego.

11. Yeyigwafile, yayilya na masoli

12. Inyengo ing'angafu (inzugi) yadenyekye muluwono

13. Mfumbika moto muhenge chusi kilaling'a

14. Apanya makukilo peyitonyite indonya

15. Imbwa sakwinava se sesisele

Thursday, July 28, 2022

UMUYAGO YE MWIYENDA

 Umuyago ye mwiyenda mamaa

Umyago ye mwiyenda

Umuyago ye mwiyenda mama ye muhavi mulala

Gendeluwema mama

Gendeleuwema

Gendeluwema mama munyi yavene

Wednesday, July 27, 2022

HIVI UNAJUA WAHEHE WALITOKEA WAPI? FUATILIA HAPA

Isimila

 Tukirudi nyuma kama miaka 11,000 iliyopita tuna ushahidi kuwa walikuweko binadamu ambao walitumia silaha za kuchonga mawe, kihistoria zama hizo hujulikana  kama zama za mawe au stone age era.

 Kilomita chache kutoka mji wa Iringa, ukiwa unaelekea  na barabara kuu iendayo Mbeya, kuna sehemu inaitwa Isimila,

hapa katika bonde moja kubwa kunapatikana ushahidi wa vipande vya mawe vilivyochongwa kwa ajili ya kazi mbalimbali hasa za uwindaji katika zama hizo.

Wahehe walipopafahamu hapa ndipo wakapaita Isimila, jina linalotokana na neno la Kihehe ‘simo’, maana yake fumbo. Kwani kuweko kwa silaha zile za mawe kwa wahehe lilikuwa fumbo.

Ukiingia sehemu za Usagala kuna mlima uitwao Ikombagulu, huku kuna pango ambako iko michoro ya zamani sana, kuonyesha kuwa pia kulikuwa na watu waliokuwa na utamaduni wa michoro ya mapangoni.

Katika bhonde la mto Lya Ndembela kuna ushahidi wa kuishi watu ambao Wahehe katika simulizi zao waliwaitwa Vanyidaha,

 watu hawa waliacha ushahidi wa utamaduni uliofanana sana na utamaduni wa Wairaki wa huko Mbulu, kuna watafiti wanasema wakazi hao walikuwa Wairaki wa zamani.

 Baadhi ya utamaduni waliouacha Wairak hawa ni kulima kando ya mito maarufu kwa jina la finyungu, na kutumia mawe ya kutoka mtoni kusagia nafaka.  Wahehe waliendeleza utamaduni huu na huita mawe hayo nunulilo.

Pia walikuwa na utamaduni wa kujenga majengo ya mviringo kutumia mawe,mpaka miaka ya mwanzoni ya 60 kulikuwa na mabaki ya jengo la namna hiyo kule Kiwiluka, ambalo lilikuja fumuliwa taratibu na watoto. Kule Engaruka, Monduli kulikuwa na mabaki ya majengo ya aina hiyohiyo.

Katika bonde hilo la Lyambangali kulikuwa na masalia ya majengo mengine, yaliyojengwa kwa matofali ya kuchomwa. Wahehe katika simulizi zao za kale walisema waliojenga nyumba hizo walikuwa Waiyenzele,

 Ugogoni kulikuwa na masalia ya majengo kama hayo na Wagogo walisimulia kuwa wajenzi wa magofu yale walikuwa Wamankala, lakini hakuna maelezo zaidi kuhusu watu hawa kuwa Waiyenzele au Wamankala walikuwa wa aina gani , walitoka wapi, na walienda wapi.

Watu wengine waliokuweko katika nchi hii walikuwa ni Mbilikimo. Kuna hadithi za kale za Wahehe kuwa hawa Mbilikimo walikuwa hodari kwa mishale, kwa vile walikuwa wafupi walikuwa wanawaona watu wengine mapema na kupiga kelele ‘Ngulenge’ yaani  nimekwisha kulenga.

Kama mtu alimuona Mbilikimo kwanza alimwambia , Nguwene’  maana yake nimekuona, na hawa mbilikimo, walikuwa    wakiuliza  umbonie kwi? Kwa sababu hiyo mpaka zama hizi Mbilikimo au watu wafupi Uheheni, hujulikana kwa jina la utani, Mwanangulenge au Wambonie kwi

Kundi jingine la watu waliokuweko katika uwanda huu wa Wahehe kabla ya ujio wa Wahehe walikuwa Wahamya au kwa Kiingereza huitwa Bushmen, hawa ni wafupi lakini si wafupi kama mbilikimo na pia huwa ni weupe kiasi.

Hawa walifika mpaka sehemu za Manyoni na kuanza kuchanganyika na wenyeji, wajukuu za Wahamya hawa waliobakia Uheheni huitwa kwa mwidikiso wa Mkemwa na mwiko wao (msilo), ni nyama ya pundamilia.

Ukoo wa kina Mwisaka chanzo chao ni Wahamya hawa.

Kundi la mwisho ni Vahumma, Wahehe hutamka Vahumba, ni kundi ambalo kwa  Kiingereza hujulikana kama Hamitic.

Hawa nao walienda kuweka maskani yao katika bonde la Lyambangali .


Tuesday, July 26, 2022

LIVANGALA 1


 

NDALINYELE KUUTSUNGWA BE ABE


Ndalinyele Kuutsungwa  - be abe

Ndililige tunutunu -be abe

Twaanige datsudatsu - be abe

Nda kagombo ka Utsungwa - be abe

Wa wonige unegulile  - be abe

Nge nige negule  -be abe

Twitang'ana libohola -be abe

Likwanuka libohola -be abe

Wawonige upokapoke =be abe

Nge nige moka moke -be abe

Likwingila mugupango -be abe

Wawonige uhengahenge  -be abe

Nge ninge nyenga nyenge - be abe

Ilihengo lyadumwike  - be abe

Wawonige uponda ponde  - be abe

Nge ninge monda monde - be abe

Avaponzi vasisile -be abe

Asige yukiwale - be abe

Ya kupondaga libume - be abe

kasimo dumu



Monday, July 25, 2022

TWIYENGELIGUTUGIMBI - KUKULEKU...simo 1

 Twiyengeligu tugimbi - kukuleku

Na umuyangu kasogolo - kukuleku

Tukisindikila kwivaha - kukuleku

Vakutupela ligida - kukuleku

Tukima tukikanila - kukuleku

Vakatupela likolo -kukuleku

Tukwitumbulila katumbu - kukuleku

Tukyanikilia pi figa - kukuleku

Ikasi imbwa yi vaha - kukuleku

Kwe ihumile kwekwenula - kukuleku

Ve mbwa ve utegwe kiki -  kukuleku

Ye negwe tengefiga - kukuleku 

Wusu utengele ipa - kukuleku

Pagonile nyambuya - kukuleku

Nyambuya kidibwidibwi - kukuleku

Yakudibulagu utulenga -kukulele

Tulenga twa vanu vehe - kukulele

Kasimi dumu

KALIBUNI MULIBULOGU LYA KIHEHE

 


KUNA LIMJAMAA DE LIMBUSIGE ENE NDIWESA KUGITA  MANYI IBLOGU YA KIHEHE, SWE NIGE SAWA,  IBOLOGU IYI IPA. INO NDISUKU UMUSAADA ENE WINA IHADISI YA KIHEHE, APAMWI WINA KINU CHOCHOTE WISAKA KIWONEKANE MU BLOGU IYI, VE NZANDIKILE NEKE NDETELE MU WATSAP 0713274747.... ALE  NYELA KINU IKI IPA TUVANGI IKASI

STAT COUNTER