Vanu velu au watu weupe waliotoka Kilwa waliingia nchi ya Uheheni kwa amani na wakaendelea kuishi kwa amani na hatimae kuwa sehemu ya wenyeji, mfano nilioutoa ni wakina Kiwhele.
Lakini kuna kundi jingine la
watu weupe hawa waliingia kutoka kaskazini na kuingia katika eneo lililoitwa
Ugunda, wenyeji wa Ugunda walikuwa ni Wategeta, habari zao nilikwisha
zizungumzia awali. Jina la Ugunda lilitokana na babu yao mmoja aliyeitwa
Mugunda. Eneno la Ugunda kwa sasa
linaitwa Image na tutaelezana chanzo cha jina hilo baadae. Kama mnakumbuka, niliwaeleza
kuwa Wategeta walikuwa wafua chuma wazuri sana na walikuwa watu walioishi kwa
mpangilio mzuri katika kazi yao hiyo, pia niliwaambia kuwa walikuwa ni watu
wenye maungo makubwa yenye afya hawakuwa watu wa mchezo. Kuna kundi moja la
Wahumma kutokea aidha Pawaga au Izazi, liliwashambulia Wategeta hawa ili
kuwanyang’anya ng’ombe. Pamoja na Wahuma kuwa na silaha za kutisha ,Wategeta
waliwakamata adui zao hao kwa mikono na kuanza kuwachanachana vipande.
Walimbakiza Muhumba mmoja tu nae walikata masikio wakamwachia aende kwao
akahadithie. Baada ya hapo Wategeta wakawa mara kwa mara wanawashambulia Wahuma
na kuwanyang’anya ng’ombe bila upinzani mkubwa.
Lakini hili kundi la watu weupe kutoka kaskazini liliwazidi sana nguvu
Wategeta. Wenyeji wengi wakalazimika kukimbia nchi yao na kukimbilia upande wa
iliko Pawaga sasa, wale maadui waliwafwata mpaka huko na kuwamaliza na
waliobaki kuwachukua watumwa na kwenda kuwauza Pwani. Mahala palipokamilisha
vita hiyo palikuja kuitwa Malikilo maana yake pa kumalizia. Siku hizi panaitwa
Kidali.
Wategeta
wengine walikimbia kaskazini na kufika mpaka ulipo sasa mpaka wa Kenya na
Uganda. Huko wakalikuta kabila la Wasamia na kuwashinda na kuwa watawala wao.
Hata siku hizi wajukuu zao hujiita Bahehe na kusema kuwa babu zao walitokea
Uheheni. Kundi jingine la Wategeta lilikimbilia Mahenge na baadae kuanza
kufuata bonde la Kilombelo kisha kuingia
Ubena na kuendelea na safari hadi Kaskazini mwa Ziwa Nyasa, wakaanza kuishi
sehemu waliyoiita Kavala, maana yake
peupe penye kuwaka jua, wakaendelea na kazi yao ya asili ya uhunzi.
Wengi wao walikuwa wa ukoo wa kina Chusi na wakawa watawala, jina lao likageuka
kuwa Chusa, Wagonde wakaligeuza jina
hilo kuwa Wanyachusa, au Wanyakyusa. Kuna Wanyakyusa ambao hatimae walirudi
Uheheni kwa mfano ukoo wa akina Kalinga, hawa walitumia majina kama
Kwilengilyova, yaani maji yangurumayo, wakikumbuka maporomoko ya maji katika sehemu walizopita
wakati wakisafiri wakifuata bonde la Kilombelo. Wengine wakijiita Magalamatitu,
wakikumbuka sehemu ambapo kulikuwa tambarare
ya ndege wengi weusi ambayo ipo
mpaka leo. Hawa watu weupe waliowafukuza Wategeta waliacha uzao wao katika nchi
ya Usagala. Wajukuu hawa wa Wasagala wa zamani, ambao hujulikana kama
Vanyikami, huwa na madai tofauti, wengine wakidai kuwa asili yao ni waarabu,
wengine wakidai asili yao ni wazungu. Wanahistoria wengi huona hiyo si rahisi
kwani wangekuwa Waarabu, lazima wangeanzisha dini ya Kiislamu na hali kadhalika
wangekuwa wazungu kungeletwa pia ukristu. Kinachodhaniwa ni kuwa Vanu velu hawa
walikuwa ni machotara au watu tu wenye ngozi angavu.
Mimina
ReplyDeleteTwiga kwa Kihehe ni Nundulu au Singomlanzi kwa mujibu wa sisi Wana Image.
ReplyDelete