Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, November 18, 2012

WANAKIHESA WACHANGA ZAIDI YA MILIONI MBILI

Kikao cha matayarisho ya siku ya Wanakihesa 2/12/2012, inayotegemewa kufanyika Makumbusho Dar es Salaam kimekuwa cha mafanikio makubwa kwa wajumbe kuwa wengi zaidi, wajumbe wamezidi kufanikisha michango yao,na kuwa mpaka sasa zimekusanywa zaidi ya shilingi milioni mbili na nusu. Leo tena  kikao kilichangamka sana kikiwa na wajumbe wengi zaidi akiwemo Brown Mbigili, ambaye aliburudisha kikao kwa kutukumbusha Rais wa Kihesa…Mtambule marehemu Mzee Mbigili. Picha za kikaoNo comments:

Post a Comment