Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, December 2, 2012

MATUKIO KIHESA DAY 1Mkunungu


Baada ya matayarisho ya siku ya Wanakihesa kwa miezi kadhaa , hatimae ndoto ya Wanakihesa ilitimia kwa siku hiyo kuweko na mamia ya wanaKihesa na wanaIringa kwa ujumla kujitokeza katika siku hii iliyojaa furaha, na kumbukumbu nyingi. Kama ilivyokuwa imepangwa katika vikao vya awali siku ya Wanakihesa ilikuwa ni siku ya wahusika kuonyesha shughuli zao mbalimbali katika siku hii. Hivyo basi wapishi walipika chakula na kuuza, wabunifu walileta vifaa vyao zikiwemo nguo na mapambo ya asili, watengenezaji wa sabuni walileta mali zao, kulikuweko na walioleta vyakula kama bagia za Iringa ambazo ziliisha mapema sana kama ilivyoisha mikusu na matundadamu, na mkunungu. Picha zifuatazo zilionyesha kazi mbalimbali za wajasilia mali wa Kihesa wakiwemo, book publishers waliokuja kuonyesha vitabu vya aina mbalimbali.

No comments:

Post a Comment