Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Wednesday, November 14, 2012

18/11/2012 SIKU YA MKUTANO MUHIMU KWA WANAKIHESA

MwanaKihesa Mage
Jumapili tarehe 18/11 kuna kikao muhimu kwa Wanakihesa, Wanakihesa wote mnakaribishwa kwenye kikao hiki cha maandalizi. kama kawaida kikao kitakuwa KGB Hotel Riverside kuanzia saa 9 mchana, tutangaziane.
Matangazo ya sherehe yetu ya mwezi Desemba yataanza katika Clouds Radio wiki hii, na yaendelea hadi kilele cha  siku muhimu ya siku ya Wanakihesa mwanzoni mwa Desemba.

No comments:

Post a Comment