Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Tuesday, October 23, 2012

PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE na MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI


MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI
 Mwana Kihesa huyu, alikuwa pilot wa ndege wa kwanza kutoka Kihesa, hii ilikuwa  mwanzoni mwa 1970. Mwamba alikuwa ni mtoto pekee wa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa Mzee Mnyamwani Kasongo. Mzee huyu mwenye asili ya ya mji wa  Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo alitinga Kihesa mwishon wa miaka ya 50.  Ukoo huu ilizimika duniani baada ya  Mwamba, Mama Mwamba, Mzee Mnyamwani, na mkee wake wa pili Binti Mussa wote kutangulia mbele ya haki. 

++++++++++++++++++++++++++++++++++
 PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE
 Mwana Kihesa huyu mtoto wa mama Se Uhagile ni msomi aliyebobea na ni muhadhiri pale chuo cha SAU ama kwa hakika kama si Profesor pekee toka Kihesa basi ni mmoja wa maprofesor wachache toka Kihesa. Alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugalo katika miaka ya 70, alikuwa  na tabia ya kusoma sana na pale alipotaka kupumzika basi rafiki zake wakubwa walikuwa Edson Mwamwani, Anderson Mwanyato na Ahmed Wanguvu wakitumia muda wao kucheza Bumping kwa wimbo wa Kung Fu Fighting, hapo ni mpaka jasho liwatoke.

No comments:

Post a Comment