Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Tuesday, October 23, 2012

MATAYARISHO YA SIKU YA WANAKIHESA YAPAMBA MOTO

Katika kikao cha wanaKihesa cha kutayarisha siku ya wanakihesa tarehe 2/12/2012, wanaKihesa waliokusanyika siku hiyo waliweza kukusanya shilingi laki saba cash. Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuwa kikao kijacho  cha tarehe 4/11/2012 kuwa ni muhimu sana watu wengi kufika kwani ndicho kitatoa picha kamili ya maandalizi ya ya tamasha.
 Pia tarehe 22/10/2012 matangazo ya tamasha yata anza kurushwa hewani rasmi na vituo vya Country Fm Iringa, na siku chache baadae vituo vya Clouds na Radio Free Africa vitaanza kutangaza taarifa za tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment