Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Tuesday, October 23, 2012

SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO na ANDERSON ZABRON MWANYATO


 SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO ni mwana Kihesa  ambaye pia ni mkurugenzi wa MAJEMBE AUCTION MART ni mtoto wa kwanza wa mmoja wa wazee waanzilishi wa kihesa  Methusela Mwamotto .
 Setti ameajiri vijana, wazee na wakina mama wengi kutoka Kihesa kwenye kampuni yake ya Majembe. Setti amekuwa akijitolea kujenga na kukarabati makanisa, misikiti na kuwasaidia kwa matibabu, misiba , na kadhalika ya watu wengi wa Iringa.
    
  ANDERSON  ZABRON MWANYATO, mwanafunzi wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ndugu Philip Mangula ni msomi wa darasa la 7 tu. lakini mambo aliyoyafanya enzi za uhahi wake ni kama mtu mwenye PHD. Anderson Mwanyato ni mtoto wa 4 wa mama Sekinyunyu na Mzee Z.K Mwanyato.
 Ndiye alikuwa mkurugenzi wa Comfort Enterprises
ambayo inamiliki hotel ya Comfort Kitonga, akishirikiana na ndugu zake wawili hayati Joshua na Alex. Alitoa mchango mkubwa wa kijamii mkoani Iringa
 Mdogo wake Robert anasema anamkumbuka kwa kuwa mtu wa kuweza kushaurika, kwani yeye ndiye aliyemshauri ujenzi ule wa hotel porini  Wanamuziki Hayati Ndala Kasheba na King kiki ndio waliosindikizana na Robert ili kupiga katika uzinduzi wa hoteli ile 1993. Comfort hotel ipo chini ya mkurugenzi pekee  aliyebaki hai, Alex Zabron Mwanyato.

No comments:

Post a Comment