Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Tuesday, October 16, 2012

WAJUE WAZEE WA KIHESA 6


MZEE ERNEST MWANDANZI 
 Mzee huyu Mhehe wa Mufindi aliyestaafu uaskari akiwa na cheo cha Inspekta, ni mmoja wa wanzilishi wa Kihesa, alifanikiwa kuwa moja ya madiwani wa eneo hili.  Mzee Ndanzi ndiye baba mzazi wa Gerald Ndanzi wa Majembe Auction Mart.

MZEE MARTIN MLOWE 
 Mzee huyu Mbena  wa Kifanya - Njombe  ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa. Pamoja na kujishughulisha na kilimo eneo la Mangao Ismani, aliku.wa na bucha  pale Kihesa alibarikiwa kupata watoto wengi kama Gaspar, Oscar, Gerard, mtoto wa mwisho wa kiume Afred Mlowe alikuwa mchezaji kiungo wa Kihesa Stars, mchezaji mwenzie Robert Nyato hudai kuwa anamfananisha na Steven Gerald Alfred ndiye mtunza hazina wa Umoja wa wana Kihesa. Kwa sasa ni mfanyakazi wa Manispaa ya kinondoni 

Leo tutazungumzia wasifu wa wazee wa kihesa ambao ni wazazi wa ndugu Faustini Mdesa cosmas na tutamzungumzia Mzee wa kijana mhamasishaji wa siku ya wana kihesa  Ali mduba.

MZEE COSMAS MDESA
 Mzee huyu Mhehe wa Ifunda ni mwana Kihesa ambaye alijishughulisha na kilimo huko Kihologota Ismani akiwa na mjomba wake mzee Mwang’ingo. Mzee huyu ndiye baba mzazi wa mwenyekiti wa maandalizi ya siku ya wana kihesa Ndugu Faustine Cosmas Mdesa

MZEE JIMMY MWAMBAGO
 Mzee huyu Mbena wa Njombe ambaye alitinga Kihesa 1962, akitokea Tanga ambako alikuwa akifanya kazi upimaji na ramani. Mzee Jimmy alijiunga na kufanya kazi TANCUT na kusaafu mwishoni mwaka 1979. Bingwa huyu ambaye ni mzazi wa mwenyekiti wa Mkusanyiko wa wana Kihesa wa dar es Salaam Ndugu Nordrick Mwambago. Kwa sasa mzee Mwambago bado yupo anaishi Kihesa nyumbani kwake. Mwanae  Nodrick Jimmy Mwambago ndie  mwenyekiti wa wana KIHESA na mwenyekiti wa  kamati ya maandalizi ya siku ya wana Kihesa 2/12/2012

No comments:

Post a Comment