Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Tuesday, October 16, 2012

KABATI KATIBA STAR SEARCH YAPATA 20 BORA

Jumamosi tarehe 13 Oktoba katika ukumbi wa Welfare Center, mambo makubwa mawili yalifanyika, kwanza vijana wengi walioshiriki na wale waliokuja kufuatia Kabati Katiba Star Search walipata elimu nzuri ya Katiba ya Tanzania. Na pili ilikuwa burudani kwa kwenda mbele kutoka kwa vijana walioshiriki Star Search kuonyesha vipaji vyao. Vijana 150 waliweza kujitokeza kuonekana mbele ya jopo la majaji
majaji  Eddo Bashir (Ebony Fm), Temmy Mahondo (Country Fm), Dj Ammy Yeyo (Country Fm ), Agnes Anderson (Ebony Fm) na Dj Muba wa (Ebony Fm) . Mchujo uiofanyika baada ya hapo uliwezesha vijana 20 kuingia katika Top Twenty ya mpambano huo. Tarehe 27 Oktoba ndipo itakapoingia awamu ya pili ya shindano hili na Top Ten kupatikana.

No comments:

Post a Comment