Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Friday, October 12, 2012

WAZEE WA KIHESA-5-MZEE RUBENI NYALUSI

Klerruu
Mzee huyu Mbena wa Lupembe alikuwa fundi stadi wa ujenzi na kuongoza umoja wa wajenzi Kihesa yeye akiwa mwenyekiti. Mzee huyu pia alijishughulisha na kilimo sehemu za Ngano Ismani, sambamba na Mzee Philipo Sawani. Hayati Mzee Nyalusi ndiye baba mzazi wa mchezaji mahiri wa ile timu maarufu Kihesa Stars Simoni Nyalusi.
Mchezaji huyu aliyekuwa na vituko vingi uwanjani, mpaka hivi leo bado yupo Kihesa akijishughulisha na ufundi ujenzi. Miongoni mwa vituko ambavyo mtoa habari hii Bwana Robert Nyato anasema hatasahau ni kitendo cha kupewa kadi nyekundu na refarii baada ya kumvuta pua mshika kibendera marehemu Bruda Modestus katika mechi kati ya Kihesa Stars na Lipuli zote za Iringa, refa  Mzee Maselenge alimtoa nje. Kituko kingine ni akiwa kama mtazamaji kwenye mashindano ya vyuo pale Kleruu aliingia uwanjani na kuifungia bao timu ya Kleruu na kusababisha mchezo kusimama takribani dakika 20 na wachezaji wa  timu ile ya Chuo cha Mbeya kuanza kumfukuza Simoni bila mafanikio yoyote.

No comments:

Post a Comment