Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Friday, October 5, 2012

ENDELEA KUIJUA HISTORIA YA KIHESA

 WASIFU WA WAZEE WAANZILISHI WA KIHESA

 (1) MZEE JUMBE OMARY  
  Huyu mzee makazi yake ya mwanzo yalikuwa Kigonzile, baadae aliamia Kihesa karibu na mlima lilipo  kanisa la Kilutheli la Kihesa. alichaguliwa kuwa JUMBE,
Kazi yake aliamua kesi mbalimbali na kuwahamisha watu kuja eneo ilipo Kihesa kutoka  milimani, kwa mfano mlima Mafifi.
Kesi zilizo mshinda alizipeleka Kalenga wakati huo ndiko kulikwepo mahakama ya mwanzo. Mwandishi wa habari hii alimuona Mzee JUMBE OMARY mara ya mwisho mwishoni mwa miaka ya 1970. Alikuwa na ngeu usoni ambayo inasemekana  aliwahi kupigana na simba.

(2) AZIZA SEMGENI
 
 Bibi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa, yeye alikuwa anatibu kwa miti shamba, Eneo lake ndipo palipo jegwa shule ya msingi Kihesa. Wajukuu wa Bibi Aziza ni Mzee Jonas Mgeni ( Baba Zacho) Mzee Lwinusu Mgeni (Baba Riziki)

(3) SEMTEMA KUUKINGA
Mama huyu wa kabila la Kikinga aiifariki miaka michache aliopita ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa na alikuwa anamiliki eneo ambalo mpaka leo maarufu kwa jina la SEMTEMA  karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Tumaini

(4) SALUMU SOSOVELE
Huyu mzee kwa waliobahatika kumuona alikuwa pandikizi la mtu. mwenye kuongea kwa tabasamu. Baba yake mzazi ndie aliyemiliki eneo kilipo jegwa Chuo Cha Elimu Kleruu.Na kaburi la baba wa Salum lipo jirani na Kanisa Katoliki Kihesa.

1 comment:

  1. Katika utafiti ambao nimekuwa nikiufanya katika kipindi cha miaka 8 kuhusu chimbuko na kuzagaa kwa Ukoo wa Kivenule, ulioenea katika sehemu za Nduli, Mugongo, Itagutwa, Irore, Igominyi, Isimani, Kalenga, Nzihi, Kidamali, Magubike, Idete, Nyamihuu, Idodi na Pawaga. Inaamini baadhi ya Watoto wa Tavimyenda Tagumtwa (Balama) Kivenule, waliozaliwa kwa Bibi Senosa, waliishi maeneo ya Kihesa. Hawa ni Bibi Malibora Tavimyenda Kivenule, Babu Abdalah Tavimyenda Kivenule na Bibi Sigungilimembe Tavimyenda Kivenule. Kuna uhusiano wa karibu baina ya Kivenule na akina Balama. Katika Mkutano Mkuu wa Ukoo wa Kivenule uliopangwa kufanyika Juni 29-30, 2013 Kijijini Kidamali, tunapanga kuwaalika akina Balima toka sehemu hizo nilizotaji na wale wanaotoka Mjini Iringa ili tuweze kupata kiundani kuhusiana na uhusiano huu baina ya hizo koo mbili. Kwa taarifa na mawasiliano: Adam Kivenule, Katibu wa Umoja wa Ukoo wa Kivenule (KAUKI), Simu: 0713 270364, E-mail: kivenule@gmail.com / kauki2006@gmail.com na blog www.tagumtwa.blogoak.com / www.kauki-kauki.blogspot.com

    ReplyDelete