Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Friday, October 5, 2012

WANAKIHESA WAONGEZEA MAJINA YA WAANZILISHI WA KIHESA

-->

Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa waongezwe hawa:

1.   Mzee Mtwivila,
2.     Fabian,
3.    Bibi Semtema,
4.    Mzee Lwaho,
5.     Victo Mwibalama,
6.     Mzee Mwambua (Baba Mussa),
7.     Mzee Ally Ngimba,
8.    Edward Wissa,
9.    Mgeni (Baba Jenifa),
10.                Kavilwa (Mourise),
11.                Msigomba,
12.               Balama (Baba Vero),
13.                Balama (mnyakilabu),
14.                Kibassa (Baba John),
15.               King Miking Kibassa (Babu yangu),
16.                Mzee Ng'owo,
17.                Ngogo (Mwanji),
18.               Tenga's wote (kuanzia Ngimonyi hadi wengine),
19.                Kalinga (Baba Moses),
20.               Nyalusi (Baba Mercy wa Timber),
21.                Mgeni (MZALENDO),
22.               Kigahe,
23.               G.G. Shambe,
24.               John Mbegalo,
25.               Gwegime (watoto wake hadi leo machampion),
26.                Sambala (Baba Marcelino),
27.               Mzee Luhanga (Baba yake Mwanyenza),
28.               Mzee Cheka (Baba ya Cheka Club Semtema),
29.                Mzee Gohage (Babu Fredy),
30.               Mzee James (Baba Baldo),
31.                Mwanzo Mgumu (Chao),
32.                Abel Lulandala (Baba Aidan),
33.                Fivawo,
34.               Mzee Kisonga.
 Pia orodha bado ni ndefu sana TUSAIDIANE KUIBORESHA

2 comments:

 1. Hii blog pamoja na umoja wa wanakihesa nimevipenda. tafadhali nifahamishwe mkutano mwingine au tujadili jinsi ya kuuandaa tena....

  anuani yangu: nguzofa@gmail.com

  ReplyDelete
 2. Pia ongezeni majina yafuatayo:
  1. Mzee Saidi Nguzo (Baba Khalid wa Tan Cut Club)
  2. Musa Sabuli (Baba Stumai)
  3. Mzee Upete (dereva wa magari ya relwe)
  4. Sheikh Ibrahim Mwiginga (fundi maarufu wa saa pale sokoni)
  5. Bwana Mikate (jina silikumbuki; jirani yake Kandanda)
  6. Mandondo Gawolile (Baba Anna; fundi nguo maarufu kihesa, alinishonea uniform wakati naanza la kwanza kichangani mwaka 1969)
  7. Biti Alubati (alikuwa na kilabu pale transfoma; Bibi yake Mwache)
  8. Mahundi (pia fundi nguo maarufu kihesa, vile vile kiongozi wa kikundi cha ngoma ya mganda, kilikuwa kikitoa burdani pale sokoni siku za jumapili saa za alasiri. Kilitia fora sana na kuongeza ladha ya maisha ya kihesa)
  9. Mzee Saidi Majani
  10. Mzee Shabani (Maarufu kwa jina la Shabani makopo; alikuwa fundi wa kuripea sufuria, ndoo, madebe, taa za chemli, koroboi n.k.)

  ReplyDelete