Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, October 7, 2012

WAZEE WA KIHESA -2-MZEE ISAYA KIGAHE

MFARANYAKI CLUB
Mzee huyu wa kabila la Kibena ambaye mpaka leo yupo pale Kihesa, ni mmoja ya wazee waliofika eneo la Kihesa miaka ya 1940. Ukiachaa mwanae wa kwanza Gerald Isaya Kigahe ambaye amefariki miezi michache iliyopita, Mzee huyu alikuwa na mwanae  aliyeitwa Naftari Isaya Kigahe aliyefariki takribani miongo miwili iliyopita. Naftari  alikuwa JEMBE kwa wana kihesa, huyu bwana ndio mmoja wa wawaanzilishi wa lile eneo la Mkimbizi ki ujenzi na likaitwa kwa Kigahe. Moja ya vitu ambavyo vilimgalimu Naftari kuanza kukaa eneo hili ni kuvamiwa na majambazi na kupigwa risasi, aliuguwa na kupona majeraha na kuendelea na shughuli zake kama kawaida. 
Naftari Kigahe ndiye mwenye watoto akiwemo Rogers, Christina, Ganma na mkewe se Msamba maarufu Mama Kigahe bado yupo, Mkimbizi kwa Kigahe anaendesha biashara zake. Kwa waliosoma shule ya msingi ya Chemchem , miaka hiyo ikiitwa Consolata Primary school watamkumbuka Naftari kuwa alikuwa ndiye alikuwa mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule miaka hiyo. Bendi iliyokuwa chini ya Mwalimu Daudi Luhanga.

No comments:

Post a Comment