Tuesday, October 23, 2012
PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE na MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI
MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI
Mwana Kihesa huyu, alikuwa pilot wa ndege wa kwanza kutoka Kihesa, hii ilikuwa mwanzoni mwa 1970. Mwamba alikuwa ni mtoto pekee wa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa Mzee Mnyamwani Kasongo. Mzee huyu mwenye asili ya ya mji wa Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo alitinga Kihesa mwishon wa miaka ya 50. Ukoo huu ilizimika duniani baada ya Mwamba, Mama Mwamba, Mzee Mnyamwani, na mkee wake wa pili Binti Mussa wote kutangulia mbele ya haki.

++++++++++++++++++++++++++++++++++
PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE
Mwana Kihesa huyu mtoto wa mama Se Uhagile ni msomi aliyebobea na ni muhadhiri pale chuo cha SAU ama kwa hakika kama si Profesor pekee toka Kihesa basi ni mmoja wa maprofesor wachache toka Kihesa. Alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugalo katika miaka ya 70, alikuwa na tabia ya kusoma sana na pale alipotaka kupumzika basi rafiki zake wakubwa walikuwa Edson Mwamwani, Anderson Mwanyato na Ahmed Wanguvu wakitumia muda wao kucheza Bumping kwa wimbo wa Kung Fu Fighting, hapo ni mpaka jasho liwatoke.
MATAYARISHO YA SIKU YA WANAKIHESA YAPAMBA MOTO
Katika kikao cha wanaKihesa cha kutayarisha siku ya wanakihesa tarehe 2/12/2012, wanaKihesa waliokusanyika siku hiyo waliweza kukusanya shilingi laki
saba cash. Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuwa kikao kijacho cha tarehe 4/11/2012 kuwa ni
muhimu sana watu wengi kufika kwani ndicho kitatoa picha kamili ya maandalizi
ya ya tamasha.
Pia tarehe 22/10/2012 matangazo ya tamasha yata anza kurushwa hewani rasmi na vituo vya Country Fm Iringa, na siku chache baadae vituo vya Clouds na Radio Free Africa vitaanza kutangaza taarifa za tamasha hilo.

SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO na ANDERSON ZABRON MWANYATO
SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO ni mwana Kihesa ambaye pia ni mkurugenzi wa MAJEMBE AUCTION MART ni
mtoto wa kwanza wa mmoja wa wazee waanzilishi wa kihesa Methusela
Mwamotto .
Setti ameajiri vijana, wazee na wakina mama wengi kutoka Kihesa kwenye kampuni yake ya Majembe. Setti amekuwa akijitolea kujenga na kukarabati makanisa, misikiti na kuwasaidia kwa matibabu, misiba , na kadhalika ya watu wengi wa Iringa.

ANDERSON ZABRON MWANYATO, mwanafunzi wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ndugu Philip Mangula ni msomi wa darasa la 7 tu. lakini mambo aliyoyafanya enzi za uhahi wake ni kama mtu mwenye PHD. Anderson Mwanyato ni mtoto wa 4 wa mama Sekinyunyu na Mzee Z.K Mwanyato.
Ndiye alikuwa mkurugenzi wa Comfort
Enterprises
ambayo inamiliki hotel ya Comfort Kitonga, akishirikiana na ndugu zake wawili hayati Joshua na Alex. Alitoa mchango mkubwa wa kijamii mkoani Iringa
Mdogo wake Robert anasema anamkumbuka kwa kuwa mtu wa kuweza kushaurika, kwani yeye ndiye aliyemshauri ujenzi ule wa hotel porini Wanamuziki Hayati Ndala Kasheba na King kiki ndio waliosindikizana na Robert ili kupiga katika uzinduzi wa hoteli ile 1993. Comfort hotel ipo chini ya mkurugenzi pekee aliyebaki hai, Alex Zabron Mwanyato.

Tuesday, October 16, 2012
WAJUE WAZEE WA KIHESA 6
MZEE ERNEST MWANDANZI
Mzee huyu Mhehe wa Mufindi aliyestaafu uaskari akiwa na cheo cha Inspekta, ni mmoja wa wanzilishi wa Kihesa, alifanikiwa kuwa moja ya madiwani wa eneo hili. Mzee Ndanzi ndiye baba mzazi wa Gerald Ndanzi wa Majembe Auction Mart.

MZEE MARTIN MLOWE
Mzee huyu Mbena wa Kifanya - Njombe ni
mmoja wa waanzilishi wa Kihesa. Pamoja na kujishughulisha na kilimo eneo la
Mangao Ismani, aliku.wa na bucha
pale Kihesa alibarikiwa kupata watoto wengi kama Gaspar, Oscar, Gerard,
mtoto wa mwisho wa kiume Afred Mlowe alikuwa mchezaji kiungo wa Kihesa Stars,
mchezaji mwenzie Robert Nyato hudai kuwa anamfananisha na Steven Gerald Alfred
ndiye mtunza hazina wa Umoja wa wana Kihesa. Kwa sasa ni mfanyakazi wa Manispaa
ya kinondoni
Leo
tutazungumzia wasifu wa wazee wa kihesa ambao ni wazazi wa ndugu Faustini Mdesa
cosmas na tutamzungumzia Mzee wa kijana mhamasishaji wa siku ya wana
kihesa Ali mduba.
MZEE COSMAS MDESA
Mzee huyu Mhehe wa Ifunda ni mwana Kihesa ambaye alijishughulisha na kilimo huko Kihologota Ismani akiwa na mjomba wake mzee Mwang’ingo. Mzee huyu ndiye baba mzazi wa mwenyekiti wa maandalizi ya siku ya wana kihesa Ndugu Faustine Cosmas Mdesa
MZEE JIMMY MWAMBAGO
Mzee huyu Mbena wa Njombe ambaye alitinga Kihesa 1962, akitokea Tanga ambako alikuwa akifanya kazi upimaji na ramani. Mzee Jimmy alijiunga na kufanya kazi TANCUT na kusaafu mwishoni mwaka 1979. Bingwa huyu ambaye ni mzazi wa mwenyekiti wa Mkusanyiko wa wana Kihesa wa dar es Salaam Ndugu Nordrick Mwambago. Kwa sasa mzee Mwambago bado yupo anaishi Kihesa nyumbani kwake. Mwanae Nodrick Jimmy Mwambago ndie mwenyekiti wa wana KIHESA na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya siku ya wana Kihesa 2/12/2012

KABATI KATIBA STAR SEARCH YAPATA 20 BORA
Jumamosi tarehe 13 Oktoba
katika ukumbi wa Welfare Center, mambo makubwa mawili yalifanyika, kwanza vijana wengi walioshiriki na wale
waliokuja kufuatia Kabati Katiba Star Search walipata elimu nzuri ya Katiba ya
Tanzania. Na pili ilikuwa burudani kwa kwenda mbele kutoka kwa vijana
walioshiriki Star Search kuonyesha vipaji vyao. Vijana 150 waliweza kujitokeza
kuonekana mbele ya jopo la majaji
majaji Eddo Bashir (Ebony Fm), Temmy Mahondo (Country
Fm), Dj Ammy Yeyo (Country Fm ), Agnes Anderson (Ebony Fm) na Dj Muba wa (Ebony
Fm) . Mchujo uiofanyika baada ya hapo uliwezesha vijana 20 kuingia katika
Top Twenty ya mpambano huo. Tarehe 27 Oktoba ndipo itakapoingia awamu ya pili
ya shindano hili na Top Ten kupatikana.
Friday, October 12, 2012
WAZEE WA KIHESA-5-MZEE RUBENI NYALUSI
![]() |
Klerruu |
Mchezaji huyu aliyekuwa na vituko vingi uwanjani, mpaka hivi leo bado yupo Kihesa akijishughulisha na ufundi ujenzi. Miongoni mwa vituko ambavyo mtoa habari hii Bwana Robert Nyato anasema hatasahau ni kitendo cha kupewa kadi nyekundu na refarii baada ya kumvuta pua mshika kibendera marehemu Bruda Modestus katika mechi kati ya Kihesa Stars na Lipuli zote za Iringa, refa Mzee Maselenge alimtoa nje. Kituko kingine ni akiwa kama mtazamaji kwenye mashindano ya vyuo pale Kleruu aliingia uwanjani na kuifungia bao timu ya Kleruu na kusababisha mchezo kusimama takribani dakika 20 na wachezaji wa timu ile ya Chuo cha Mbeya kuanza kumfukuza Simoni bila mafanikio yoyote.
WAZEE WA KIHESA-4-MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO
-->
Mzee huyu Mbena wa Kidegembye alitinga kihesa 1935. kwa miaka kadhaa aliishi
nyuma ya mlima Mafifi kabla ya kuja kuwa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa. Kabla hajajulikana kama
mkulima stadi alikuwa fundi washi, ndipo baadae akajishughulisha na kilimo kupitia mashamba makubwa aliokuwa nayo maeneo ya Chamdindi na Kifuluto kule Isimani.
Mzee huyu akiwa na mkewe mama Sekinyunyu alifikia uwezo wa kumiliki magari na matrekta. Mtoto wake wa kwanza alikuwa Waston maarufu kwa jina la Fwasi Kilega ambaye kwa sasa ni marehemu na wengine kama Matata(Mbinu), Geofrey, Manase, Yotema wapo bado Kihesa mpaka leo.

Thursday, October 11, 2012
KABATI KATIBA STAR SEARCH- KUZINDULIWA JUMAMOSI
Katika kuhamasiisha vijana wa
Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika
kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM
Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua KABATI KATIBA STAR SEARCH. Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya
Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha,
na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili
kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA
STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo
mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya
kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne
na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba
vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii
inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa
wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.
Tuesday, October 9, 2012
MSIBA KIHESA CHRISTOPHER MMASI HATUNAE TENA
CHRISTOPHER MMASI KAKA WA PATRICIA MMASI AMEFARIKI USIKU HUU HUKO IRINGA. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMINA
KWA MICHANGO MBALIMBALI YA RAMBIRAMBI UNAWEZA KUTUMA KUPITIA SIMU NAMBA 0754591929-DEVOTA MSILUTAARIFA ZIMELETWA NA ROBERT MWANYATO
INDONYA NGOMI KUMWANI TWIYANGALILE
Kwa kuwa wameweka kidhungu ngoja tuweke Kiswahili kwa kifupi, TAHADHARI
YA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI, KATI YA 8TH OKTOBA NA 11 OKTOBA 2012.
MAENEO HUSIKA NI MIKOA YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, PWANI, NA VISIWA VYA
UNGUJA NA PEMBA. KUNAWEZEKANA KUWEKO NA MVUA KUBWA YA KATI YA 50mm na
100mm KATIKA KIPINDI CHA MASAA 24,
Monday, October 8, 2012
WAZEE WA KIHESA 3- MZEE LOTTI LUPEMBE
-->
Mzee huyu wa kabila
la Kibena alikuwa mkulima wa kawaida sehemu za Isimani kama ilivyokuwa
kawaida ya wazee wengi waanzilishi wa Kihesa. Baada ya mavuno mazuri
walijenga nyumba zao Kihesa. Mzee
lotti alijizolea umaarufu Kihesa kwa tabia yake ya kujitolea kupita
asubuhi na mapema karibu kila mtaa na kutoa matangazo kwa wananchi , kwa mfano
mtoto kapotea, ama kuna msiba umetokea n.k, kutokana na umaarufu huo wa Mzee
Lotti, pale kihesa kuna mtaa unaitwa kwa LOTTI LUPEMBE .
Sunday, October 7, 2012
WAZEE WA KIHESA -2-MZEE ISAYA KIGAHE
![]() |
MFARANYAKI CLUB |
Naftari Kigahe ndiye mwenye watoto akiwemo Rogers, Christina, Ganma na mkewe se Msamba maarufu Mama Kigahe bado yupo, Mkimbizi kwa Kigahe anaendesha biashara zake. Kwa waliosoma shule ya msingi ya Chemchem , miaka hiyo ikiitwa Consolata Primary school watamkumbuka Naftari kuwa alikuwa ndiye alikuwa mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule miaka hiyo. Bendi iliyokuwa chini ya Mwalimu Daudi Luhanga.
WAZEE WA KIHESA -1-MZEE PHILIPO SAWANI
Mzee huyu wa kabila la Kikinga ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa alikuwa mkulima eneo la Ngano Isimani. Huku akiendesha biashara ya
duka na bar hapo KIHESA katika nyumba yake ya kisasa kabisa. Wazee matajiri wa
mji wa Iringa mfano Mzee Mwaitebele, Mzee Idd Mwangubi, Mzee Zabron Mwanyato
pamoja na wafanya kazi maofisa kama Mzee Asam Sajio Kaduma walipenda kunywa
kwenye bar ya Mzee Sawani. Lakini pia alipokuwa Mwenyekiti wa Tanganyika African Parents Association (TAPA) wa
wilaya na alinunua jengo kwa pesa zake na kulifanya shule ya TAPA ambayo kwa sasa
inaitwa Shule ya Msingi Mtwivila. Na mwalimu wa shule hiyo wa kwanza alikuwa Mwalimu Edward Chaula ( Baba Kichupa ) na Joseph Msandi ambao mishahara yao ililipwa na mzee
Philipo Sawani. Jully Sawani ni mtoto wa Mzee Sawani ambaye alikuwa diwani
wa kwanza Kihesa. Mzee Sawani alikuwa mtu nadhifu sana
akipendelea kuvaa English suit. Ama kwa hakika Mzee Philipo Sawani ana mambo
mengi sana aliyochangia kwa Kihesa na maisha ya wengi tukisema tuyaandike yote hapatoshi.
Friday, October 5, 2012
WANAKIHESA WAONGEZEA MAJINA YA WAANZILISHI WA KIHESA
-->
Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa waongezwe hawa:
Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa waongezwe hawa:
1. Mzee Mtwivila,
2. Fabian,
3. Bibi Semtema,
4. Mzee Lwaho,
5. Victo Mwibalama,
6. Mzee Mwambua (Baba Mussa),
7. Mzee Ally Ngimba,
8. Edward Wissa,
9. Mgeni (Baba Jenifa),
10.
Kavilwa (Mourise),
11.
Msigomba,
12.
Balama
(Baba Vero),
13.
Balama (mnyakilabu),
14.
Kibassa (Baba John),
15.
King
Miking Kibassa (Babu yangu),
16.
Mzee Ng'owo,
17.
Ngogo (Mwanji),
18.
Tenga's
wote (kuanzia Ngimonyi hadi wengine),
19.
Kalinga (Baba Moses),
20.
Nyalusi
(Baba Mercy wa Timber),
21.
Mgeni (MZALENDO),
22.
Kigahe,
23.
G.G.
Shambe,
24.
John
Mbegalo,
25.
Gwegime
(watoto wake hadi leo machampion),
26.
Sambala (Baba Marcelino),
27.
Mzee
Luhanga (Baba yake Mwanyenza),
28.
Mzee
Cheka (Baba ya Cheka Club Semtema),
29.
Mzee Gohage (Babu Fredy),
30.
Mzee
James (Baba Baldo),
31.
Mwanzo Mgumu (Chao),
32.
Abel Lulandala (Baba Aidan),
33.
Fivawo,
34.
Mzee
Kisonga.
Pia
orodha bado ni ndefu sana TUSAIDIANE KUIBORESHA
ENDELEA KUIJUA HISTORIA YA KIHESA
WASIFU WA WAZEE WAANZILISHI WA KIHESA
(1) MZEE JUMBE OMARY
Huyu mzee makazi yake ya mwanzo yalikuwa Kigonzile, baadae aliamia Kihesa karibu na mlima lilipo kanisa la Kilutheli la Kihesa. alichaguliwa kuwa JUMBE,
Kazi yake aliamua kesi mbalimbali na kuwahamisha watu kuja eneo ilipo Kihesa kutoka milimani, kwa mfano mlima Mafifi.
Kesi zilizo mshinda alizipeleka Kalenga wakati huo ndiko kulikwepo mahakama ya mwanzo. Mwandishi wa habari hii alimuona Mzee JUMBE OMARY mara ya mwisho mwishoni mwa miaka ya 1970. Alikuwa na ngeu usoni ambayo inasemekana aliwahi kupigana na simba.
(2) AZIZA SEMGENI
Bibi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa, yeye alikuwa anatibu kwa miti shamba, Eneo lake ndipo palipo jegwa shule ya msingi Kihesa. Wajukuu wa Bibi Aziza ni Mzee Jonas Mgeni ( Baba Zacho) Mzee Lwinusu Mgeni (Baba Riziki)
(3) SEMTEMA KUUKINGA
Mama huyu wa kabila la Kikinga aiifariki miaka michache aliopita ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa na alikuwa anamiliki eneo ambalo mpaka leo maarufu kwa jina la SEMTEMA karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Tumaini
(4) SALUMU SOSOVELE
Huyu mzee kwa waliobahatika kumuona alikuwa pandikizi la mtu. mwenye kuongea kwa tabasamu. Baba yake mzazi ndie aliyemiliki eneo kilipo jegwa Chuo Cha Elimu Kleruu.Na kaburi la baba wa Salum lipo jirani na Kanisa Katoliki Kihesa.

Wednesday, October 3, 2012
WAZEE MAARUFU WALIOIJENGA KIHESA
- MZEE JUMBE OMARY
- MZEE LOTTI LUPEMBE
- MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO
- MZEE PHOLIPO SAWANI
- MZEE RUBEN NYARUSI
- MZEE ANDREW MKOCHA
- MZEE METUSALA SINZIA MWAMOTTO
- MZEE NIKOLAI CHAWE
- MZEE PESAMBILI RAIS
- MZEE JUMANNE MWANDAMIZI
- MZEE JIMMY MWAMBAGO
- MZEE CAPRO MAHANJAM MDEGELA
- MZEE JOHN MAUYA
- MZEE FEDRICK KIHADE
- MZEE SHEM MAINGARA
- MZEE VICENT MSEMWA MFARANYAKI
- MZEE LUBAFU LWASOMBA
- MZEE ELEUTEL KIMILIKE
- MZEE RUPI SABA MKUSA
- MZEE GARUS KING'UNZA
- MZEE GARUS MWANYAKUNGA
- MZEE JAMES CHOMI
- MZEE WILLIAM MNG'ONG'O
- MZEE MATHAYO MNG'ONG'O
- MZEE METUSALA MNG'ONG'O
- MZEE PETER MSILU
- MZEE EDWARD MMASI
- MZEE GEORGE SAWALA
- MZEE LUCAS MKUSA
- MZEE MUSSA MWACHANG'A
- MZEE AUGUSTINO MWACHANG'A
- MZEE EMMANUEL MWACHANG'A
- MZEE MARTIN MLOWE
- MZEE JOHN NZALI BALANCE
- MZEE MKINGA SAFI MBILINYI
- MZEE AMOSI MPOGOLE
- MZEE SAID KITENGE
- SHEKHE MDOKA MAULID
- SHEKHE SAID KALELA
- SHEKHE SAID WANGUVU
- MAMA DIANA MAGRETH
- MZEE MPOGOLE (BABA SAREHE)
- MZEE ALEX SANGA
- MZEE ISAYA KAGAHE
- MZEE SAMSON NYATO
- MZEE SAMWEL KINYUNYU
- MZEE MALIO MSILU
- MZEE HAMISI KINGENG'ENA
- MZEE NGAIRO( BABA STIVIN)
- MZEE KUDINGWA MAPUNDA
- MZEE FRANSIS KITIME
- MZEE LAMEKI TUMBUKA
- MZEE IBRAHIM MWIBARAMA
- MZEE KALYIEMBE ( BABA ANYWELWISE)
- MZEE SIXMUND MOLAMOLA
- MZEE JOSEPH KASUMRI SANGA
- MZEE MKULU EZEKIA
- MZEE CHODOTA (BABA ELIABI)
- MZEE MTEVELA (BABA FOIDA)
- MZEE OBADIA NGOGO
- MZEE PETER NGWIVAHA
- MZEE EDWARD MAKWETA
- MZEE ADAMU KAPUNGU
- MZEE ELIEZA MNG'ONG'O
- MZEE EDSON MWAMWANI
- MZEE JOHN LUSUNDE
- MZEE ZABRON KINYAMAGOHA
- MZEE EPHRANI KILATU
- MZEE SALUM NYENZI
- MZEE ADAM SAJIO KADUMA
- MZEE JONASI MGENI
- MZEE ZAKARIA CHUWA
- MZEE MAIGE MACHIBYA
- MZEE KUFAKUNOGA MAHAMODU
- MZEE PETER LUPEMBE
- MZEE LINGWENDU SANGA
- MZEE JOHN KANYWENDA
- MZEE MARTINE MWAMBILINGE
- MZEE AMRAN MDEMU
- MZEE HENRY NYANYEMBE
- MZEE JOHN LUHANGA
- ZABRONI LUVINGA
- MZEE ALI MDUBA
- MZEE MARKO MFUGALE
- MZEE ALFREDY MBATA
- MZEE JOHN GILIKI
- MZEE JOHN EJO
- MZEE GALAHENGA BEATUSI
- MZEE MDENDEMI
- MZEE MWANYWAEGE
- MZEE DANIEL LUGENGE
- MZEE KIDUNU
- MZEE MNG'ONGO'
- MZEE MBILINYI
- MZEE MWANANGUNULE
- MZEE KANDANDA
- MZEE TITIKOO
- MZEE SALUM MDEGIPARA
- MZEE FUNGO
- MZEE MGOMBELE
- MZEE NZELU
- MZEE KIDULILE
- MZEE MBIFILE
- MZEE ELIAS SANGA
- MZEE NGWALE
- MZEE MARTIN KIDUKO
- MZEE KIWELE
- MZEE MWITA
- MAMA GIFT
- MZEE NGALAWA (BABA MWAMBA)
- MZEE DICKS DISUZA
- MZEE MAGAVA
- MZEE FARAHANI
- MZEE BENARD MBIGILI
- MZEE POYO
- MZEE MNYAMWANI
- MZEE KAPANDE
- MZEE MWALIWELO
- MZEE MALILA
- MZEE CHENGULA
- MZEE FURAHISHA
- MZEE WILILO (BABA ROBERT)
- MZEE MASENYA
- MZEE BABA HILDA
- MZEE MASHAKA WILLBAKI
- MZEE KIKOSI JUMA MASOUD
- MZEE COSMAS MDESA
- MZEE MLIMBILA
- MZEE MBOMBWE
- MZEE SOSTEN KYANDO
- MZEE NDITI
- MZEE BABA MAYASA
- MZEE WEEK END
- MZEE LUGENGE
- MZEE LUGALA
- MZEE MWANG'INGO
- MZEE ODO
- MZEE RUNYASI
- MZEE SEKAHANGA
- MZEE MFIKWA
- MZEE AMBROS MWANGWADA
- MZEE KIWONAOMELA
- MAMA SAMAMBA
- MZEE LUCHABIKO KAPUGI
- MCHUGAJI CHUSI
- MZEE MACHILINA
- MAMA SEMPOGOLE
- MAMA GEORGE KUMBEMBA MWAKIMBENGONDO MGODAGWIVAHA MUNYIDUNDA
- MZEE SAMUEL BWANANGONDO M.M MWAKIMBE
NB: KUNA WAZEE WASIOPUNGUA 200 WALIO IJENGA KIHESA TUTAENDELEE KUSAIDIANA KUWAKUMBUKA KAMA MAJINA YAO HAYAPO HAPA
KATIKA MAANDALIZI YA SIKU YA WANA KIHESA TUTAKUWA TUNAWACHAMBUA WASIFU WA WAZEE HAWA.
IMETAYARISHWA NA ROBERT
MWANYATO: MRATIBU WA TAMASHA LA WANA KIHESA
Subscribe to:
Posts (Atom)