Kwa kuwa wameweka kidhungu ngoja tuweke Kiswahili kwa kifupi, TAHADHARI
YA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI, KATI YA 8TH OKTOBA NA 11 OKTOBA 2012.
MAENEO HUSIKA NI MIKOA YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, PWANI, NA VISIWA VYA
UNGUJA NA PEMBA. KUNAWEZEKANA KUWEKO NA MVUA KUBWA YA KATI YA 50mm na
100mm KATIKA KIPINDI CHA MASAA 24,
Tuesday, October 9, 2012
Monday, October 8, 2012
WAZEE WA KIHESA 3- MZEE LOTTI LUPEMBE
-->
Mzee huyu wa kabila
la Kibena alikuwa mkulima wa kawaida sehemu za Isimani kama ilivyokuwa
kawaida ya wazee wengi waanzilishi wa Kihesa. Baada ya mavuno mazuri
walijenga nyumba zao Kihesa. Mzee
lotti alijizolea umaarufu Kihesa kwa tabia yake ya kujitolea kupita
asubuhi na mapema karibu kila mtaa na kutoa matangazo kwa wananchi , kwa mfano
mtoto kapotea, ama kuna msiba umetokea n.k, kutokana na umaarufu huo wa Mzee
Lotti, pale kihesa kuna mtaa unaitwa kwa LOTTI LUPEMBE .
Sunday, October 7, 2012
WAZEE WA KIHESA -2-MZEE ISAYA KIGAHE
![]() |
MFARANYAKI CLUB |
Naftari Kigahe ndiye mwenye watoto akiwemo Rogers, Christina, Ganma na mkewe se Msamba maarufu Mama Kigahe bado yupo, Mkimbizi kwa Kigahe anaendesha biashara zake. Kwa waliosoma shule ya msingi ya Chemchem , miaka hiyo ikiitwa Consolata Primary school watamkumbuka Naftari kuwa alikuwa ndiye alikuwa mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule miaka hiyo. Bendi iliyokuwa chini ya Mwalimu Daudi Luhanga.
WAZEE WA KIHESA -1-MZEE PHILIPO SAWANI
Mzee huyu wa kabila la Kikinga ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa alikuwa mkulima eneo la Ngano Isimani. Huku akiendesha biashara ya
duka na bar hapo KIHESA katika nyumba yake ya kisasa kabisa. Wazee matajiri wa
mji wa Iringa mfano Mzee Mwaitebele, Mzee Idd Mwangubi, Mzee Zabron Mwanyato
pamoja na wafanya kazi maofisa kama Mzee Asam Sajio Kaduma walipenda kunywa
kwenye bar ya Mzee Sawani. Lakini pia alipokuwa Mwenyekiti wa Tanganyika African Parents Association (TAPA) wa
wilaya na alinunua jengo kwa pesa zake na kulifanya shule ya TAPA ambayo kwa sasa
inaitwa Shule ya Msingi Mtwivila. Na mwalimu wa shule hiyo wa kwanza alikuwa Mwalimu Edward Chaula ( Baba Kichupa ) na Joseph Msandi ambao mishahara yao ililipwa na mzee
Philipo Sawani. Jully Sawani ni mtoto wa Mzee Sawani ambaye alikuwa diwani
wa kwanza Kihesa. Mzee Sawani alikuwa mtu nadhifu sana
akipendelea kuvaa English suit. Ama kwa hakika Mzee Philipo Sawani ana mambo
mengi sana aliyochangia kwa Kihesa na maisha ya wengi tukisema tuyaandike yote hapatoshi.
Friday, October 5, 2012
WANAKIHESA WAONGEZEA MAJINA YA WAANZILISHI WA KIHESA
-->
Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa waongezwe hawa:
Katika hii orodha ya wazee wa Kihesa waongezwe hawa:
1. Mzee Mtwivila,
2. Fabian,
3. Bibi Semtema,
4. Mzee Lwaho,
5. Victo Mwibalama,
6. Mzee Mwambua (Baba Mussa),
7. Mzee Ally Ngimba,
8. Edward Wissa,
9. Mgeni (Baba Jenifa),
10.
Kavilwa (Mourise),
11.
Msigomba,
12.
Balama
(Baba Vero),
13.
Balama (mnyakilabu),
14.
Kibassa (Baba John),
15.
King
Miking Kibassa (Babu yangu),
16.
Mzee Ng'owo,
17.
Ngogo (Mwanji),
18.
Tenga's
wote (kuanzia Ngimonyi hadi wengine),
19.
Kalinga (Baba Moses),
20.
Nyalusi
(Baba Mercy wa Timber),
21.
Mgeni (MZALENDO),
22.
Kigahe,
23.
G.G.
Shambe,
24.
John
Mbegalo,
25.
Gwegime
(watoto wake hadi leo machampion),
26.
Sambala (Baba Marcelino),
27.
Mzee
Luhanga (Baba yake Mwanyenza),
28.
Mzee
Cheka (Baba ya Cheka Club Semtema),
29.
Mzee Gohage (Babu Fredy),
30.
Mzee
James (Baba Baldo),
31.
Mwanzo Mgumu (Chao),
32.
Abel Lulandala (Baba Aidan),
33.
Fivawo,
34.
Mzee
Kisonga.
Pia
orodha bado ni ndefu sana TUSAIDIANE KUIBORESHA
ENDELEA KUIJUA HISTORIA YA KIHESA
WASIFU WA WAZEE WAANZILISHI WA KIHESA
(1) MZEE JUMBE OMARY
Huyu mzee makazi yake ya mwanzo yalikuwa Kigonzile, baadae aliamia Kihesa karibu na mlima lilipo kanisa la Kilutheli la Kihesa. alichaguliwa kuwa JUMBE,
Kazi yake aliamua kesi mbalimbali na kuwahamisha watu kuja eneo ilipo Kihesa kutoka milimani, kwa mfano mlima Mafifi.
Kesi zilizo mshinda alizipeleka Kalenga wakati huo ndiko kulikwepo mahakama ya mwanzo. Mwandishi wa habari hii alimuona Mzee JUMBE OMARY mara ya mwisho mwishoni mwa miaka ya 1970. Alikuwa na ngeu usoni ambayo inasemekana aliwahi kupigana na simba.
(2) AZIZA SEMGENI
Bibi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa, yeye alikuwa anatibu kwa miti shamba, Eneo lake ndipo palipo jegwa shule ya msingi Kihesa. Wajukuu wa Bibi Aziza ni Mzee Jonas Mgeni ( Baba Zacho) Mzee Lwinusu Mgeni (Baba Riziki)
(3) SEMTEMA KUUKINGA
Mama huyu wa kabila la Kikinga aiifariki miaka michache aliopita ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa na alikuwa anamiliki eneo ambalo mpaka leo maarufu kwa jina la SEMTEMA karibu kabisa na Chuo Kikuu cha Tumaini
(4) SALUMU SOSOVELE
Huyu mzee kwa waliobahatika kumuona alikuwa pandikizi la mtu. mwenye kuongea kwa tabasamu. Baba yake mzazi ndie aliyemiliki eneo kilipo jegwa Chuo Cha Elimu Kleruu.Na kaburi la baba wa Salum lipo jirani na Kanisa Katoliki Kihesa.

Subscribe to:
Posts (Atom)