SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO ni mwana Kihesa ambaye pia ni mkurugenzi wa MAJEMBE AUCTION MART ni
mtoto wa kwanza wa mmoja wa wazee waanzilishi wa kihesa Methusela
Mwamotto .
Setti ameajiri vijana, wazee na wakina mama wengi kutoka Kihesa kwenye
kampuni yake ya Majembe. Setti amekuwa akijitolea kujenga na kukarabati
makanisa, misikiti na kuwasaidia kwa matibabu, misiba , na kadhalika ya watu
wengi wa Iringa.
ANDERSON ZABRON MWANYATO, mwanafunzi wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ndugu Philip Mangula ni
msomi wa darasa la 7 tu. lakini mambo aliyoyafanya enzi za uhahi wake ni kama
mtu mwenye PHD. Anderson Mwanyato ni mtoto wa 4 wa mama
Sekinyunyu na Mzee Z.K Mwanyato.
Ndiye alikuwa mkurugenzi wa Comfort
Enterprises
ambayo inamiliki hotel ya Comfort Kitonga, akishirikiana na ndugu zake wawili
hayati Joshua na Alex. Alitoa mchango mkubwa wa kijamii mkoani Iringa
Mdogo wake Robert anasema anamkumbuka kwa kuwa mtu wa kuweza kushaurika,
kwani yeye ndiye aliyemshauri ujenzi ule wa hotel porini Wanamuziki Hayati Ndala Kasheba na King
kiki ndio waliosindikizana na Robert ili kupiga katika uzinduzi wa hoteli ile
1993. Comfort hotel ipo chini ya mkurugenzi pekee aliyebaki hai, Alex Zabron Mwanyato.