Katika kuhamasiisha vijana wa
Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika
kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM
Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua KABATI KATIBA STAR SEARCH. Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya
Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha,
na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili
kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA
STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo
mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya
kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne
na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba
vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii
inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa
wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.
Thursday, October 11, 2012
Tuesday, October 9, 2012
MSIBA KIHESA CHRISTOPHER MMASI HATUNAE TENA
CHRISTOPHER MMASI KAKA WA PATRICIA MMASI AMEFARIKI USIKU HUU HUKO IRINGA. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMINA
KWA MICHANGO MBALIMBALI YA RAMBIRAMBI UNAWEZA KUTUMA KUPITIA SIMU NAMBA 0754591929-DEVOTA MSILUTAARIFA ZIMELETWA NA ROBERT MWANYATO
INDONYA NGOMI KUMWANI TWIYANGALILE
Kwa kuwa wameweka kidhungu ngoja tuweke Kiswahili kwa kifupi, TAHADHARI
YA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI, KATI YA 8TH OKTOBA NA 11 OKTOBA 2012.
MAENEO HUSIKA NI MIKOA YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, PWANI, NA VISIWA VYA
UNGUJA NA PEMBA. KUNAWEZEKANA KUWEKO NA MVUA KUBWA YA KATI YA 50mm na
100mm KATIKA KIPINDI CHA MASAA 24,
Monday, October 8, 2012
WAZEE WA KIHESA 3- MZEE LOTTI LUPEMBE
-->
Mzee huyu wa kabila
la Kibena alikuwa mkulima wa kawaida sehemu za Isimani kama ilivyokuwa
kawaida ya wazee wengi waanzilishi wa Kihesa. Baada ya mavuno mazuri
walijenga nyumba zao Kihesa. Mzee
lotti alijizolea umaarufu Kihesa kwa tabia yake ya kujitolea kupita
asubuhi na mapema karibu kila mtaa na kutoa matangazo kwa wananchi , kwa mfano
mtoto kapotea, ama kuna msiba umetokea n.k, kutokana na umaarufu huo wa Mzee
Lotti, pale kihesa kuna mtaa unaitwa kwa LOTTI LUPEMBE .
Sunday, October 7, 2012
WAZEE WA KIHESA -2-MZEE ISAYA KIGAHE
![]() |
MFARANYAKI CLUB |
Naftari Kigahe ndiye mwenye watoto akiwemo Rogers, Christina, Ganma na mkewe se Msamba maarufu Mama Kigahe bado yupo, Mkimbizi kwa Kigahe anaendesha biashara zake. Kwa waliosoma shule ya msingi ya Chemchem , miaka hiyo ikiitwa Consolata Primary school watamkumbuka Naftari kuwa alikuwa ndiye alikuwa mpiga ngoma kubwa katika bendi ya shule miaka hiyo. Bendi iliyokuwa chini ya Mwalimu Daudi Luhanga.
WAZEE WA KIHESA -1-MZEE PHILIPO SAWANI
Mzee huyu wa kabila la Kikinga ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa alikuwa mkulima eneo la Ngano Isimani. Huku akiendesha biashara ya
duka na bar hapo KIHESA katika nyumba yake ya kisasa kabisa. Wazee matajiri wa
mji wa Iringa mfano Mzee Mwaitebele, Mzee Idd Mwangubi, Mzee Zabron Mwanyato
pamoja na wafanya kazi maofisa kama Mzee Asam Sajio Kaduma walipenda kunywa
kwenye bar ya Mzee Sawani. Lakini pia alipokuwa Mwenyekiti wa Tanganyika African Parents Association (TAPA) wa
wilaya na alinunua jengo kwa pesa zake na kulifanya shule ya TAPA ambayo kwa sasa
inaitwa Shule ya Msingi Mtwivila. Na mwalimu wa shule hiyo wa kwanza alikuwa Mwalimu Edward Chaula ( Baba Kichupa ) na Joseph Msandi ambao mishahara yao ililipwa na mzee
Philipo Sawani. Jully Sawani ni mtoto wa Mzee Sawani ambaye alikuwa diwani
wa kwanza Kihesa. Mzee Sawani alikuwa mtu nadhifu sana
akipendelea kuvaa English suit. Ama kwa hakika Mzee Philipo Sawani ana mambo
mengi sana aliyochangia kwa Kihesa na maisha ya wengi tukisema tuyaandike yote hapatoshi.
Subscribe to:
Posts (Atom)