MZEE Jackson Mvangila Makweta, Mbunge wa Njombe wa muda mrefu (1975-2000), na Mzee
aliyewahi kushika nafasi ya kadhaa za Uwaziri katika serikali ya Tanzania amefariki jioni
hii katika hospitali ya Muhimbili kutokana na matatizo ya Moyo Mungu Amlaze
pema peponi Amen
Saturday, November 17, 2012
Thursday, November 15, 2012
Wednesday, November 14, 2012
18/11/2012 SIKU YA MKUTANO MUHIMU KWA WANAKIHESA
MwanaKihesa Mage |
Matangazo ya sherehe yetu ya mwezi Desemba yataanza katika Clouds Radio wiki hii, na yaendelea hadi kilele cha siku muhimu ya siku ya Wanakihesa mwanzoni mwa Desemba.
Sunday, November 11, 2012
MSIBA MWINGINE KIHESA
MwanaKihesa Ahmed Wanguvu amefiwa na mama yake mchana wa tarehe 11/11/2012 Kihesa Iringa. Mazishi yatakuwa tarehe 12/11/2012. Kwa kutoa salamu za rambirambi unaweza kutumia namba za Ahmed 0754 319850 na 0767 290300.
Mungu amlaze mama yetu pema peponi
Mungu amlaze mama yetu pema peponi
Wednesday, November 7, 2012
PICHA YA WIKI--WANAKIHESA
Hii ilikuwa mwaka 1989 TANCUT HALL mbele ni Robert K Mwanyato na nyuma yake ni DC wa Kibonda Mr Venance Sethi Mwamoto kumbukumbu safiii
Sunday, November 4, 2012
KIKAO CHA WANAKIHESA CHAFANA

Moja ya mambo yaliyofurahisha katika kikao ni kuwepo kwa wajukuu wa Mzee Mfaranyaki Cilla na Kidunu, kweli mkusanyiko huu umekuwa wa furaha kubwa kwani kuna wengi wanaokutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi , wengine kukutana kwa mara ya kwanza toka walipokuwa watoto, ni furaha tu. Wadau mnakaribishwa katika kikao kijacho katika tarehe iliyotajwa, katika ukumbi wa hoteli ya KGB pale Riverside Ubungo.
Thursday, November 1, 2012
MZEE MBIGILI AFARIKI DUNIA LEO 1/11/2012 JIJINI DAR ES SALAAM
WAZEE WETU WOTE HAWA WAWILI SASA NI MAREHEMU. MZEE MBIGILI AKIWA KWENYE KOTI JEUSI NA PADRI MWOGOFI. MZEE MBIGILI AMEFARIKI LEO 1/11/2012 SAA NNE ASUBUHI JIJINI DAR ES SALAAM. TARATIBU ZINAFANYIKA ILI KUWEZA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KWENDA IRINGA KESHO.
MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI AMEN
Subscribe to:
Posts (Atom)