Hii ilikuwa mwaka 1989 TANCUT HALL mbele ni Robert K Mwanyato na nyuma yake ni DC wa Kibonda Mr Venance Sethi Mwamoto kumbukumbu safiii
Wednesday, November 7, 2012
Sunday, November 4, 2012
KIKAO CHA WANAKIHESA CHAFANA

Moja ya mambo yaliyofurahisha katika kikao ni kuwepo kwa wajukuu wa Mzee Mfaranyaki Cilla na Kidunu, kweli mkusanyiko huu umekuwa wa furaha kubwa kwani kuna wengi wanaokutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi , wengine kukutana kwa mara ya kwanza toka walipokuwa watoto, ni furaha tu. Wadau mnakaribishwa katika kikao kijacho katika tarehe iliyotajwa, katika ukumbi wa hoteli ya KGB pale Riverside Ubungo.
Thursday, November 1, 2012
MZEE MBIGILI AFARIKI DUNIA LEO 1/11/2012 JIJINI DAR ES SALAAM
WAZEE WETU WOTE HAWA WAWILI SASA NI MAREHEMU. MZEE MBIGILI AKIWA KWENYE KOTI JEUSI NA PADRI MWOGOFI. MZEE MBIGILI AMEFARIKI LEO 1/11/2012 SAA NNE ASUBUHI JIJINI DAR ES SALAAM. TARATIBU ZINAFANYIKA ILI KUWEZA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KWENDA IRINGA KESHO.
MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI AMEN
Tuesday, October 23, 2012
PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE na MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI
MWAMBA KASONGO MUNYAMWANI
Mwana Kihesa huyu, alikuwa pilot wa ndege wa kwanza kutoka Kihesa, hii ilikuwa mwanzoni mwa 1970. Mwamba alikuwa ni mtoto pekee wa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa Mzee Mnyamwani Kasongo. Mzee huyu mwenye asili ya ya mji wa Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo alitinga Kihesa mwishon wa miaka ya 50. Ukoo huu ilizimika duniani baada ya Mwamba, Mama Mwamba, Mzee Mnyamwani, na mkee wake wa pili Binti Mussa wote kutangulia mbele ya haki.

++++++++++++++++++++++++++++++++++
PROFESOR JAIROS MATOVELO MWAMPOGOLE
Mwana Kihesa huyu mtoto wa mama Se Uhagile ni msomi aliyebobea na ni muhadhiri pale chuo cha SAU ama kwa hakika kama si Profesor pekee toka Kihesa basi ni mmoja wa maprofesor wachache toka Kihesa. Alikuwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugalo katika miaka ya 70, alikuwa na tabia ya kusoma sana na pale alipotaka kupumzika basi rafiki zake wakubwa walikuwa Edson Mwamwani, Anderson Mwanyato na Ahmed Wanguvu wakitumia muda wao kucheza Bumping kwa wimbo wa Kung Fu Fighting, hapo ni mpaka jasho liwatoke.
MATAYARISHO YA SIKU YA WANAKIHESA YAPAMBA MOTO
Katika kikao cha wanaKihesa cha kutayarisha siku ya wanakihesa tarehe 2/12/2012, wanaKihesa waliokusanyika siku hiyo waliweza kukusanya shilingi laki
saba cash. Wajumbe wa kikao wamekubaliana kuwa kikao kijacho cha tarehe 4/11/2012 kuwa ni
muhimu sana watu wengi kufika kwani ndicho kitatoa picha kamili ya maandalizi
ya ya tamasha.
Pia tarehe 22/10/2012 matangazo ya tamasha yata anza kurushwa hewani rasmi na vituo vya Country Fm Iringa, na siku chache baadae vituo vya Clouds na Radio Free Africa vitaanza kutangaza taarifa za tamasha hilo.

SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO na ANDERSON ZABRON MWANYATO
SETTI METUSALA SINZIALA MWAMOTTO ni mwana Kihesa ambaye pia ni mkurugenzi wa MAJEMBE AUCTION MART ni
mtoto wa kwanza wa mmoja wa wazee waanzilishi wa kihesa Methusela
Mwamotto .
Setti ameajiri vijana, wazee na wakina mama wengi kutoka Kihesa kwenye kampuni yake ya Majembe. Setti amekuwa akijitolea kujenga na kukarabati makanisa, misikiti na kuwasaidia kwa matibabu, misiba , na kadhalika ya watu wengi wa Iringa.

ANDERSON ZABRON MWANYATO, mwanafunzi wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM ndugu Philip Mangula ni msomi wa darasa la 7 tu. lakini mambo aliyoyafanya enzi za uhahi wake ni kama mtu mwenye PHD. Anderson Mwanyato ni mtoto wa 4 wa mama Sekinyunyu na Mzee Z.K Mwanyato.
Ndiye alikuwa mkurugenzi wa Comfort
Enterprises
ambayo inamiliki hotel ya Comfort Kitonga, akishirikiana na ndugu zake wawili hayati Joshua na Alex. Alitoa mchango mkubwa wa kijamii mkoani Iringa
Mdogo wake Robert anasema anamkumbuka kwa kuwa mtu wa kuweza kushaurika, kwani yeye ndiye aliyemshauri ujenzi ule wa hotel porini Wanamuziki Hayati Ndala Kasheba na King kiki ndio waliosindikizana na Robert ili kupiga katika uzinduzi wa hoteli ile 1993. Comfort hotel ipo chini ya mkurugenzi pekee aliyebaki hai, Alex Zabron Mwanyato.

Subscribe to:
Posts (Atom)