Pages

Friday, October 12, 2012

JOHN BAKERY(RIP), MWAMBA, KITIME


WAZEE WA KIHESA-5-MZEE RUBENI NYALUSI

Klerruu
Mzee huyu Mbena wa Lupembe alikuwa fundi stadi wa ujenzi na kuongoza umoja wa wajenzi Kihesa yeye akiwa mwenyekiti. Mzee huyu pia alijishughulisha na kilimo sehemu za Ngano Ismani, sambamba na Mzee Philipo Sawani. Hayati Mzee Nyalusi ndiye baba mzazi wa mchezaji mahiri wa ile timu maarufu Kihesa Stars Simoni Nyalusi.
Mchezaji huyu aliyekuwa na vituko vingi uwanjani, mpaka hivi leo bado yupo Kihesa akijishughulisha na ufundi ujenzi. Miongoni mwa vituko ambavyo mtoa habari hii Bwana Robert Nyato anasema hatasahau ni kitendo cha kupewa kadi nyekundu na refarii baada ya kumvuta pua mshika kibendera marehemu Bruda Modestus katika mechi kati ya Kihesa Stars na Lipuli zote za Iringa, refa  Mzee Maselenge alimtoa nje. Kituko kingine ni akiwa kama mtazamaji kwenye mashindano ya vyuo pale Kleruu aliingia uwanjani na kuifungia bao timu ya Kleruu na kusababisha mchezo kusimama takribani dakika 20 na wachezaji wa  timu ile ya Chuo cha Mbeya kuanza kumfukuza Simoni bila mafanikio yoyote.

TEMBELEA KIHESA KWA PICHA 1

Kama uliwahi kuwa mkazi wa Kihesa picha hizi zitakukumbusha mengi








WAZEE WA KIHESA-4-MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO

--> Mzee huyu Mbena wa Kidegembye alitinga kihesa 1935. kwa miaka kadhaa aliishi nyuma ya mlima Mafifi kabla ya kuja kuwa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa.  Kabla hajajulikana kama mkulima stadi alikuwa fundi washi, ndipo baadae akajishughulisha na kilimo kupitia mashamba makubwa aliokuwa nayo maeneo ya Chamdindi na Kifuluto kule Isimani. 
Mzee huyu akiwa na mkewe  mama Sekinyunyu alifikia uwezo wa  kumiliki  magari na matrekta. Mtoto wake wa kwanza  alikuwa Waston maarufu kwa jina la Fwasi Kilega ambaye kwa sasa ni marehemu na wengine kama Matata(Mbinu), Geofrey, Manase, Yotema wapo bado Kihesa mpaka leo.

Thursday, October 11, 2012

KABATI KATIBA STAR SEARCH- KUZINDULIWA JUMAMOSI


 Katika kuhamasiisha vijana wa Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua  KABATI KATIBA STAR SEARCH.  Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha, na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.

Tuesday, October 9, 2012

MSIBA KIHESA CHRISTOPHER MMASI HATUNAE TENA

CHRISTOPHER MMASI KAKA WA PATRICIA MMASI AMEFARIKI USIKU HUU HUKO IRINGA. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMINA
KWA MICHANGO MBALIMBALI YA RAMBIRAMBI UNAWEZA KUTUMA KUPITIA SIMU NAMBA 0754591929-DEVOTA MSILU
TAARIFA ZIMELETWA NA ROBERT MWANYATO

INDONYA NGOMI KUMWANI TWIYANGALILE

Kwa kuwa wameweka kidhungu ngoja tuweke Kiswahili kwa kifupi, TAHADHARI YA MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI, KATI YA 8TH OKTOBA NA 11 OKTOBA 2012. MAENEO HUSIKA NI MIKOA YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, PWANI, NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA. KUNAWEZEKANA KUWEKO NA MVUA KUBWA YA KATI YA 50mm na 100mm KATIKA KIPINDI CHA MASAA 24,

STAT COUNTER