Friday, October 12, 2012
WAZEE WA KIHESA-5-MZEE RUBENI NYALUSI
![]() |
Klerruu |
Mchezaji huyu aliyekuwa na vituko vingi uwanjani, mpaka hivi leo bado yupo Kihesa akijishughulisha na ufundi ujenzi. Miongoni mwa vituko ambavyo mtoa habari hii Bwana Robert Nyato anasema hatasahau ni kitendo cha kupewa kadi nyekundu na refarii baada ya kumvuta pua mshika kibendera marehemu Bruda Modestus katika mechi kati ya Kihesa Stars na Lipuli zote za Iringa, refa Mzee Maselenge alimtoa nje. Kituko kingine ni akiwa kama mtazamaji kwenye mashindano ya vyuo pale Kleruu aliingia uwanjani na kuifungia bao timu ya Kleruu na kusababisha mchezo kusimama takribani dakika 20 na wachezaji wa timu ile ya Chuo cha Mbeya kuanza kumfukuza Simoni bila mafanikio yoyote.
WAZEE WA KIHESA-4-MZEE ZABRON KIPANDULE MWANYATO
-->
Mzee huyu Mbena wa Kidegembye alitinga kihesa 1935. kwa miaka kadhaa aliishi
nyuma ya mlima Mafifi kabla ya kuja kuwa mmoja wa waanzilishi wa Kihesa. Kabla hajajulikana kama
mkulima stadi alikuwa fundi washi, ndipo baadae akajishughulisha na kilimo kupitia mashamba makubwa aliokuwa nayo maeneo ya Chamdindi na Kifuluto kule Isimani.
Mzee huyu akiwa na mkewe mama Sekinyunyu alifikia uwezo wa kumiliki magari na matrekta. Mtoto wake wa kwanza alikuwa Waston maarufu kwa jina la Fwasi Kilega ambaye kwa sasa ni marehemu na wengine kama Matata(Mbinu), Geofrey, Manase, Yotema wapo bado Kihesa mpaka leo.
Mzee huyu akiwa na mkewe mama Sekinyunyu alifikia uwezo wa kumiliki magari na matrekta. Mtoto wake wa kwanza alikuwa Waston maarufu kwa jina la Fwasi Kilega ambaye kwa sasa ni marehemu na wengine kama Matata(Mbinu), Geofrey, Manase, Yotema wapo bado Kihesa mpaka leo.
Thursday, October 11, 2012
KABATI KATIBA STAR SEARCH- KUZINDULIWA JUMAMOSI
Katika kuhamasiisha vijana wa
Iringa kushiriki katika kutoa mchango wa mawazo kuhusu katiba mpya na pia katika
kutafuta vipaji vya vijana wa Iringa, Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM
Mheshimiwa Ritha Kabati, Jumamosi hii tarehe 13 Oktoba, atazindua KABATI KATIBA STAR SEARCH. Shughuli hiyo itaanza kwa elimu ya
Katiba itakayotolewa kwa washiriki ambao mpaka sasa 400 wamekwisha jiandikisha,
na hawa watapewa elimu kuhusu katiba iliyoko na mategemeo ya katiba ijayo ili
kuhamasisha mchango wa mawazo toka vijana wa Iringa. Washindi wa KABATI KATIBA
STAR SEARCH watapatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo nafasi ya kurekodi nyimbo
mbili na video zake, kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata nafasi ya
kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa tatu atarekodi wimbo mmoja na washindi wa nne
na wa tano watafanya wimbo mmoja kwa kushirikiana. Mheshimiwa Kabati aliomba
vijana wajitokeze kwa wingi kwani watapata mengi katika shughuli hii
inayotegemea kuchukua mwezi mmoja. Wasanii kadhaa ambao ni wenyeji wa Iringa
wamekwisha onyesha nia ya kutoa ushirikiano katika shughuli hii yote.
Tuesday, October 9, 2012
MSIBA KIHESA CHRISTOPHER MMASI HATUNAE TENA
CHRISTOPHER MMASI KAKA WA PATRICIA MMASI AMEFARIKI USIKU HUU HUKO IRINGA. MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI AMINA
KWA MICHANGO MBALIMBALI YA RAMBIRAMBI UNAWEZA KUTUMA KUPITIA SIMU NAMBA 0754591929-DEVOTA MSILUTAARIFA ZIMELETWA NA ROBERT MWANYATO
Subscribe to:
Posts (Atom)