Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Wednesday, August 4, 2010

Prefect wangu


Abbas Kandoro alikuwas prefect wangu Aga Khan Secondary, siku hizi Lugalo Secondary Iringa. Namfahamu toka enzi hizo . Nina uhakika atafaa sana kuwa Mbunge wa Kalenga. Kalenga mtakuwa mmelamba dume mkimchagua Kandoro

1 comment:

  1. Kwa kweli wanakalenga wameshindwa kupitisha bwana Kandoro kwa sababu ambazo watu ni vigumu kuelelza wazi. Nampongeza Kandoro kwa ukomavu wake wa kisiasa na inatakiwa ajipange zaidi mwaka 2015 ataupata tu huo ubunge wa jimbo la kalenga

    ReplyDelete