Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe Lilinga ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Blog hii ni sehemu ya kukutania kuelezana matamu na machungu ya Iringa kwa wakazi wa Iringa walioko na ambao waliwahi kuweko hapa. Blog hii itatupa nafasi ya kukutana kuelezana na kukumbushana yaliyotukuta katika kukutana na mji huu uliopo juu ya kilima . Karibuni.

Sunday, December 2, 2012

KIHESA DAY 3-WAZEE WA KIHESA WAPEWA TUZO

-->
Katika mambo muhimu yaliyofanyika katika siku ya Kihesa ni kutoa tuzo kwa wazee ambao kwa namna moja au nyingine waliifanya Kihesa iwe ilivyo leo. Mgeni wa Heshima na mwana Kihesa Raymond Peter Mbilinyi (Mkurugenzi TIC) alitoa Tuzo hizo za heshima;
WAZEE  KUMI WA KIHESA WALIOPEWA TUZO KATIKA SIKU YA  KIHESA (KIHESA DAY)
1.     Marehemu Mzee Jumbe Omary Mwambuma –(Muwakilishi) Obed Abdallah Jumbe Omary
2.     Marehemu Mzee Lupembe Mgopinyi-(Muwakilishi) Joseph Lotti Lupembe
3.     Mzee Lucas Vigungula Mtumbuka
4.     Marehemu Mzee Emmanuel Abraham Mwachang’a-(Muwakilishi) Sinai Emmanuel Mwachang’a
5.     Marehemu Mzee Philipo Sawani Pilla (mwakilishi) Cain Mathew Sawani
6.     Marehemu Mzee Anderson Zabron Mwanyato (Mwakilishi ) Lillian Anderson Senyatto
7.     Mr Seth Metusela Mwamotto
8.     Profesa Jailos Amos Matovelo Mwampogole( Mwakilishi) George Kimbe
9.     Marehemu Norbert Zul (Mwakilishi) Julieth Zulu
10.  Benedict Kimbisa

WAZEE WANNE WAWAKILISHI WA WAZEE WOTE KIHESA
1.     Marehemu Bernard Mtarusto Mbigili (Mwakilishi) Fredyy Bernard Mbigili
2.     Elizabeth Semsamba Kihahe (Mwakilishi) Libe Semsamba
3.      John Mauya Kihade (Mwakilishi) Emmanuel Minila Mahingila
4.     Margreth Nyagawa (Mwakilishi) mama Diana

Mzee Lucas Mtumbuka1 comment: