Raha ya shule enzi hizo kwanza ni hadithi za kutisha kama zile za mazimwi, mbwa mwitu, na ujanja wa sungura. Hakuna kusahau jinsi Wagagagigikoko walivyoweza kunitokea ndotoni. Muda wa kupumzika ,ambao pale Chechem ulijulikana kama pausi (pause????) ulitawaliwa na kila aina ya michezo kama vile 'mbinga, gololi, kiboleni, mdako... huku biashara ya misasati, mifudu, mafulusadi zikiendelea.
kulikuwa natatizo moja pale Mlandege, kile choo cha wasichana tuliambiwa kina jini, na ilikuwa lazima uvuke hapo kwenda choo cha wavulana, na kumbuka wakati huo nyuma ya choo cha wavulana kulikuwa na pori kubwa si leo ambapo kumezungukwa na nyumba. Dawa ilikuwa kujitahidi usilazimike kwenda chooni wakati wa vipindi maana utakuwa nje peke yako na jini.
Choo cha mbele ni cha wasichana na nyuma ni cha wavulana
Watu wengi waliamua kukojoa darasani kuliko kukutana na jini
No comments:
Post a Comment